Tuesday, January 29, 2013

BAADA YA JAGUER MSANII WA KIGEUGEU TOKA KENYA KUFICHA MALI ZAKE PAPARAZI WAMEZINYAKA

Hii ndio nyumba ya jaguer iliyopo Nairobi hadi sasa hajaruhusu waandishi wa habari kuingia ndani kupiga picha

Msanii jaguer ni kati ya wasanii wenye pesa nchini kenya na mara nyingi amekuwa ni msiri sana na mambo yake hasa kuzionyesha mali zake,jaguer anasema mali zake wakenya wanazijua na kuziona sasa sina sababu ya kuzianika mitaandaoni kama wafanyavyo wenzangu ambao hakuwataja majina
   
Na Kama ulikuwa hufahamu basi nataka nikujulishe Katika wasanii wanao penda magari mazuri na ya bei mbaya basi Jaguar anashika Numba 1 nchini Kenya kwa kuwa na magari mazuri na ya bei Ghali. Hii ndio Range Rover yake yenye Rangi ya Silver.


Jaguar Aliandika hivi kuhusu hii Picha .`My hood,my boys....my rover"
Msanii huyo mwenye mashabiki lukuki anamiliki magari ya kifahari sana na yenye dhamani kubwa pili ana miliki mijengo ya ya maana ukiachilia nyumba yake hii mpya iliyotumia milioni 11 za kenya.
Msanii wa muziki nchini Kenya Jaguer
Chanzo chetu ambacho kipo nairobi kimetutonya kuwa jaguer huwa ni mtu asiyependa kuzionyesha mali zake hata hivyo inasemekana kuna jirani yake ndio aliyakuta magari ya juguer yakiwa yamepaki kwa pamoja akayapiga picha na kuvujisha jambo ambalo lilimkera sana msanii huyo ambaye anasadikiwa kuwa na bifu zito na msanii mwenzie prezo.
Ukiachilia mbali magari ya kifahari na majumba anayomiliki msanii huyo pia  ana miliki daladala kibao amabzo huko kwao wanaziita matatu,Jaguer aliwahi kukaririwa akisema hana bifu na msanii mwenzie prezzo na kusisitiza huwa anamfundisha maisha tu na kumuelekeza jinsi ya kuishi kistaarabu.Hii ndio picha inayosemekana ilipigwa na jirani yake kwa siri na kuiweka kwenye mitandao
Hapa ni Magari ya kifahari ya kutembelea  msanii huyo na bei zake kumbuka bei ni kwa mujibu wa pesa ya kenya


1. A silver Range Rover Sport (Cost:8million)
2. A black Mercedes E240 (Cost:5million)
3. A beige BMW 5-Series (Cost:5million)
4. A Toyota Mark X (Cost: 2million)
Jumla Ni 20 Million kwa pesa za kenya.

No comments:

Post a Comment