Friday, January 25, 2013

BREAKING NEEEWZ!!! VURUGU KUBWA WANANCHI WAFUNGA BARABARA YA MORO, DOM ENEO LA DUMILA WACHOMA NYUMBA ZA WAGENI WACHOMA MAGARI                                                         picha na maktaba
Vurugu kubwa zinaendelea hivi sasa eneo la Dumila mkoani Morogoro, kufuatia wananchi kufunga barabara ya Morogoro Dodoma, kwa kile wanachodai kumtaka Mkuu wa Mkoa Joel Bendera kufika kuwatatulia tatizo lao la kunyang'anywa maeneo yao ya wakulima na kuwapatia wafugaji.

Wananchi hao wamegawanyika katika makundi kadhaa huku kila kundi likifunga barabara ya kuingia na kutoka eneo hilo la Dumila, ambapo wamezuia magari yote yanayopita eneo hilo kutoka moro na kotoka Dom, huku wakichoma magari na kuvunja vioo vya magari hovyo, pamoja na kuchoma moto nyumba za wageni na kuvunja vioo.

Tayari Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, ameomba udhuru kutoka katika Kikao cha wakuu wa mikoa, kilichokuwa kikiendelea mkoani Dodoma, na hivi sasa yupo njiani akielekea eneo hilo kwa nia ya kukutana na wananchi hao ili kuwasikiliza na kutatua mgogoro huo.

Mtandao huu utaendeleo kuwajuza kinachoendelea kadri habari 

zitakavokuwa

chanzo DJ SEK

No comments:

Post a Comment