Monday, January 28, 2013

BREAKING: PICHA 8 ZA LULU MAHAKAMANI LEO JAN 28 PAMOJA NA MAELEZO YA MASHARTI YA DHAMANA YAKE.


                           Lulu akiwa anaingia Mahakamani leo january                                     28/ 2013 akiwa na shauku ya kupata dhamana.

Mahakama kuu leo imetangaza dhamana ya mwigizaji Lulu lakini iwapo atatimiza masharti aliyopangiwa ambayo ni pamoja na kuwasilisha hati yake ya kusafiria, kutosafiri nje ya Dar es salaam, kujiwakilisha au kuripoti mahakamani kila siku ya kwanza ya kila mwezi pamoja na wadhamini wake wawili ambao kila mmoja adhamini kwa shilingi milioni 20 za kitanzania.
Upande wa familia ya Lulu umesema masharti yote yaliyotajwa wanaweza kuyatimiza leo leo hivyo wanasubiri tu jibu la msajili ambae ndio anatakiwa kuhakikisha hayo masharti yametimia kisha ruhusa ya kumkabidhi Lulu kwa familia yake itolewe.

.

.

.

.

   Hapa ni wakati alipocheka sana pale mwandishi mmoja wa kike ambae pia alikua akimpiga picha alipokua akimlainisha Lulu kwa maneno baada ya mwigizaji huyo kuficha uso wake alipokua akipigwa picha, alisema alikua anaumizwa macho na mwanga wa kamera.

.

.

                            Mama mzazi wa Lulu ni mwenye nguo nyeupe na nyeusi.

Dr Cheni ni mmoja ya watu waliokaribu na familia ya Lulu na ameshirikiana nayo kwa muda mrefu sana kwenye hii kesi ikiwemo kufatilia mawakili, kushughulikia dhamana na mengineyo.
Docter Cheni Msanii aliyejitowa kwa hali na mali kumsaidia lulu hadi amefanikisha
Big up docter cheni hili ndilo linalotakiwa na jamii kusaidiana muhimu sana Cheni anaamini amtowa malipo ni mungu hivyo kumsaidia lulu ni wajibu wetu hivyo kama kweli ni mkosaji basi atayakuta kwa mungu kuliko kumuhukumu wakati kati yetu hatuujui ukweli.

Picha kwa hisani ya millard ayo ambaye tupo naye hadi mwisho.

No comments:

Post a Comment