Tuesday, January 22, 2013

DHAMANA YA ELIZABETH MICHAEL (LULU) ITASIKILIZWA TAREHE 25 IJUMAA 

Moja ya picha lulu akiingia mahakamani.

 

Ile kesi inayomkabili msanii wa filamu nchini tanzania elizabeth michael (lulu) imeingia hatua nyingine.
Mahakama kuu  Kanda ya Dar es Salaam,Januari 25 mwaka huu, itasikiliza ombi la kupatiwa dhamana msanii wa Filamu nchini, Elizabeth Michael (Lulu) ambaye anakabiliwa na kesi yenye namba 125/2012 ya kumuuwa bila kukusudia   msainii mwenzake marehemu Steven Kanumba.


Moja ya picha za siku nyingi lulu akiwa ana mawazo mahaman
Ombi hilo la dhamana ambalo tayari limeishapangiwa Jaji Zainabu Mruke kuanza kulisikiliza ombi hilo wakati bado kesi yake ya msingi ya kuua bila kukusudia bado haijapangiwa tarehe ya kuanza kusikilizwa, limewasilishwa mahakamani hapo  na mawakili wa Lulu ambaye anaishi gereza la Segerea .
Mawakili hao ni pamoja na Peter Kibatara,Kenned Fungamtama ,Fulgence Massawe,mawakili hao wa Lulu wamewasilisha ombi lao chini ya kifungu cha  148(1) ,(2) Cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 2002 .
 

Hapa lulu akijadiliana jambo na mmoja wa mawakili wake
“Lulu ni mtu maarufu nchini, anaiomba mahakama hii impatie dhamana na yupo tayari kutimiza masharti ya dhamana yatakayo tajwa na mahakama hii, na anaahidi kuyatimiza masharti hayo wakati akisubiri kesi yake ya msingi ya kuua bila kukusudia itakapopangiwa tarehe ya kuanza kusikilizwa katika mahakama yako tukufu”alidai Wakili Kibatara katika hati hiyo.
Picha lulu akiwa haamini kama yamemtokea yeye


Desemba 21 mwaka jana , Hakimu Mkazi Christine Mbando wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu aliifunga kesi ya kuua bila kukusudia Lulu na kuiamishia rasmi kesi hiyo katika Mahakama Kuu, na uamuzi huo wa mahakama ulitokana na upande wa Jamhuri kumsomea maelezo ya kesi yake kwa kina mshtakiwa huyo na kuieleza mahakama kuwa wanakusudia kuleta jumla ya mashahidi tisa.
Lulu akiwa na mama yake mzazi kabla ya kufikwa na matatizo.
Akizungumza na sisi mama wa msanii lulu amesema anamuombea mwanae afanikiwe kupata dhamana hiyo huku akiwaomba watanzania wenye mapenzi mema kuzidi kumuombea mwanae ili amalize kesi yake.
Mama huyo aliendelea kusisitiza kuwa anaiomba jamii isimchukulie mwanae kama muuwaji hadi pale mahakama itakapo hukumu kesi hiyo na kujua ukweli alisema mama huyo ambaye kila wakati amekuwa ni mtu wa mawazo baada ya mwanae huyo kukumbwa na mkasa huo mzito wa kuhusiswa na kifo cha marehemu steven kanumba nyumbani kwake maaeneo ya sinza vatican.

No comments:

Post a Comment