Wednesday, January 23, 2013

FLAVIANA MATATA ATWAA TUZO YA MWANAMITINDO BORA WA AFRIKA 2012

mwanamitindo Flaviana Matata.


Tuzo aliyojishindia mwanamitindo Flaviana Matata.
Kama utaambiwa utaje majina yanayoipeperusha vyema bendera ya tanzania basi naamini hutoacha kulitaja jina la mwanadada kinara na mwenye tuzo za urembo katika nchi za watu huku yeye akitokea tanzania 

Mara nyingi Flavia amekuwa akisema anaumizwa na wanamitindo wa tanzania na kusema anaamini kuna siku kwa uwezo wa mungu atafanya kitu.
 

 Flaviana Matata.
 Mwanamitindo huyo wa kimataifa kutoka  Tanzania, Flaviana Matata ameendelea kung’ara kimataifa baaada ya kushinda tuzo ya Nigeria’s Next Super Model na kuwa mwanamitindo bora barani Afrika wa mwaka 2012 (Africa’s Most Outstanding Model 2012).


Tuzo hiyo ya heshima hutolewa kwa mwanamitindo ambaye  wanaendelea kuiletea sifa  Afrika kimataifa,,  na kwa upande wa Flaviana matata amekuwa akiiletea sifa Afrika katika chati ya juu. Mwaka jana Desemba,  Flaviana alishinda tuzo nyingine  ya uwanamintindo bora kutoka kwa diaspora ya Waafrika.


mwanamitindo Flaviana Matata.
Mwanamitindo huyo  ambaye kwa sasa makazi yake  pamoja na kufanya kazi zake za uanamitindo ni pale  New York nchini Marekani.
 
Taarifa kutoka  shirika la Wilhelmina Models,inasema  mpaka sasa flavia ameitangaza Tanzania kwa kiwango kikubwa sana kimataifa kutokana na umahiri wake katika maonyesho ya mavazi.

Nadhani sisi sote ni mashahidi toka flavia ashinde taji la Miss Universe Tanzania mwaka 2007,Amekuwa ni mtu  wakung’ara katika kona zote za dunia na hasa baada ya kumaliza katika nafasi ya sita katika mashindano ya kimataifa ya Miss Universe, huku Tanzania ikishiriki kwa mara ya kwanza.


Tuzo ya Flaviana Matata.
Ameweza kushiriki katika maonyesho ya mavazi mengi Ulaya na Amerika huku akitoa misaada mingi kwa Watanzania wenzake ambao wamekuwa na ndoto ya kufika mbali katika fani hiyo.


Kwa sasa Flaviana anaendesha taasisi yake, Flaviana Matata Foundation ambayo inasomesha watoto wa kike 16 na mwaka jana alitoa msaada wa vifaa vya kuokoa maisha kama sehemu ya kumbukumbu ya kuzama kwa meli ya MV Bukoba huku ikiwa kumbukumbu ya kifo cha mama yake mzazi katika ajali hiyo ya mwaka 1996.
 Flaviana Matata.


Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Compass Communication Tanzania Limited, Maria Sarungi Tsehai alisema kuwa wamejisikia faraja sana kwa kumvumbua mwanamitindo huyo ambaye kwa sasa anashika chati ya juu Tanzania na nje ya nchi.


Maria alisema kuwa Flaviana amedhihirisha ubora wake na mpaka sasa amepitiliza kiwango cha kuitangaza Tanzania nje ya mipaka yake, ndoto ambayo alikuwa nayo muda mrefu.


 Kusema kweli flavia ni mfano wa kuigwa kwa wasanii na wanamito wenzake.

No comments:

Post a Comment