Wednesday, January 23, 2013

HALI YA MSANII MATUMAINI ANAYEPENDA KUIGIZA NA KIWEWE NI MBAYA


Matumani katika moja ya picha zake

Taarifa zilizotufikia ni kwamba hali ya msanii wa maigizo Tanzania anayejulikana kwa jina la Matumaini  sio nzuri kutokana na kuugua sana japo haijawekwa wazi anaumwa nini haswa huko nchini Msumbiji.
 
 
Matumani ambaye ni msanii wa vichekesho nchini ambaye alivuma sana enzi zile za kaole wakiwa na msanii mwenzie kiwewe hadi kufikia watu kusema kiwewe na matumaini.
matumaini na kiwewe

Tarufa za ndani kutoka kwa mtanzania moses aishie nchini msumbiji amesema kuwa hali ya matumaini ni mbaya sana na inabadilika siku hadi siku sasa tumeona ni bora kumchangia nauli ili arudi kwanza huko ili aje atibiwe na watu wa kwao maana huku hana uangalizi mzuri alisema mose.
 
Matumaini alitimkia msumbiji kwa ajili ya kwenda kutafuta maisha huko ila hali yake imekuwa mbaya kwani anasumbuliwa na maradhi ambayo kila mmoja hakutaka kuweka wazi huku akisema hawajui zaidi ya kumuona mtanzania mwenzao anaumwa na ni jukumu lao kumsaidia kwanza kabla ya kujua anasumbuliwa na nini ,sisi tunamsaidia kwanza kama mtanzania mwenzetu sasa akija huko akienda hosptalini tutajua wote alimaliza mose mtanzania huyo anayeishi nchini msumbiji.
 
matumaini akiwa na wasanii wenzake
 Baada ya kuongea na jamaa huyo tulimpigia raisi wa shirikisho la filamu tanzania ila simu yake ilikuwa inatumika na kuamua kumpigia kaftany masud.

Akizungumza jijini Dar es Salaam mjumbe wa Bodi ya Chama cha Waigizaji Mkoa wa Kinondoni , Kaftany Masoud alisema kuwa amepokea taarifa juu ya ugonjwa wa msanii huyo ingawa haijawekwa wazi anasumbuliwa na tatizo gani mpaka sasa
"Ni kweli hali ya msanii mwenzetu si nzuri anaumwa na unajua ugonjwa wa mtu unathibitishwa na Dokta hivyo bado hatujajua anaumwa nini ila tumeipokea taarifa hiyo na juhudi zinazofanywa ili kumrudisha nyumbani " alisema Masoud
Aliongezea kuwa kwa upande wao kwa sasa wapo katika mchakato wa kuchangishana fedha kwa ajili ya matibabu ya msanii huyo atakapofika hapa nchini

The superstarstz inamtakia kila kheri msanii huyo wakati wakuja huku na tutaendelea kukujulisha kila hatua itakavyojiri.

No comments:

Post a Comment