Wednesday, January 30, 2013

HALI YA MSANII MATUMAINI NCHINI MSUMBIJI NI MBAYA SANA...AANZA KUVIMBA TUMBO NA MIGUU

Matumaini alivyo ila kwa sasa kavimba hii alipigwa akiwa anaumwa kawaida kabla ya kuanza kuvimba
Habari tulizozipokea sasa hivi kwa njia ya simu toka msumbiji ni kwamba msanii wa vichekesho nchini tanzania Tumaina martini au maarufu kwa jina Matumaini yupo katika hali mbaya ya kuumwa na anahitaji msaada wa hali na mali kuweza kufanikisha safari ya kumrudisha hapa nyumbani ili Aanze swala la matibabuAkizungumza na sisi kwa njia ya simu muda huu karama mugisha mtanzania anayeishi na kufanya kazi zake nchini msumbiji amesema hali ya msanii huyo imebadilika na kuzidi kuvimba,,,,Kiukweli kaka naomba uwajulishe watu kuwa hali ya matumaini si nzuri kama wanavyodhania hali ni mbaya sana kusema kweli hapa navyokuambia miguu imevimba tumbo ndio usiseme na nitofauti na jana au leo asubuhi sasa hii hali si nzuri bora awahiswe nyumbani maana kama ikizidi itakuwa ngumu kumrejesha huko kwani kwasasa hawezi hata kutembea,alisema bwana mugisha

Msanii Matumaini hapa kabla hajaumwa
Baada ya hapo tulizungumza na mwenyekiti wa sanii Ndugu Maiki Sangu ambae amekiri kuambiwa juu ya hali hiyo na kusema ndio wapo kwenye mikakati ili wafanikishe haraka kumrejesha hapa nyumbani  kweli hali ya matumaini ni mbaya na anahitaji msaada wa hali na mali kuweza kumrudisha hapa nyumbani ,akizungumza na the super stars tz  Maiki sangu  amesema kuwa matumaini anasumbuliwa na ugonjwa wa kuvimba tumbo pamoja na miguu,na  amewataka watanzania wenye mapenzi mema na msanii huyo basi watowe chochote walicho nacho ili tuweze kumrudisha hapa nyumbani kisha taratibu za kumtibu zitaanza kwani  kila dakika tunapokea ujumbe toka huko msumbiji ukisema hali yake inazidi kuwa mbaya jambo linalotuumiza kwani hatujui kama anapata huduma yoyote kwa sasa alisema kiongozi huyo wa chama cha wasanii
.Mwenyekiti huyo wawasanii amesema kwa yeyote mwenye chochote awakilishe mchango wake kenye namba  ya simu ambayo  0718 -951-355 tigo pesa ambayo ataipokea mwenyekiti mwenyewe bwana maiki sangu.

Hapa akiwa na kiwewe Maeneo ya lidaz club kipindi hicho kwenye tamasha la wasanii
Matumani ambaye alielekea kufanya shoo huko msumbiji akiwa na wenzake ila inasemekana alipata mshikaji kule na kuamua kuweka kambi na kuwaruhusu wenzake warudi bongo akizunguza na sisi mmoja wawasanii walioenda na matumaini kule alisema wao ilikuwa ngumu kumuacha kule lakini matumaini aliwahakikishia kuwa yupo salama na pia yule shemeji yao wanajuana siku nyingi na walikutana mbeya kilisema chanzo hicho kilichoomba kisitajwe jina kuhofia kuvuruga mambo yake na wasanii wenzake

Matumaini kama utakumbuka ni kati ya wasichana waliomua kujiingiza katika fani ya vichekesho na kufiti sana haswa alipokuwa akiigiza na msanii mwenzie  kiwewe,the super stars tz inawaomba wadau na wapenzi wa filamu nchini au hata nchi za nnje ambao wanafuatilia kazi za wasanii wetu kuwa huu ni wakati wakuonyesha ushirikiano kwa binadamu mwenzetu ili aweze kupata tiba,nadhani wadau utakubaliana na mi kuwa tumekuwa tukikuhabarisha juu ya matukio ya wasanii kwa ukaribu sana sasa pia hili naomba nililete kwenu mujitowe kama mlivyojitowa kwa wengine, Ni dhahiri kuwa hatunacha kuwalipa ila mungu atasimama na nyinyi kwa kila mtakachotowa na kuwalipa msichokitegemea.

Hapa akiwa kazini
Kiukweli sikieni tu ila dada yetu yupo katika hali mbaya sana na sasa naambiwa tumbo linazidi kuwa kubwa tu na miguu imejaa maji,ila kwa uwezo wa mungu naamini atapata nguvu nasi kwa pamoja tutawezesha kurudi kwake na kumpa matibabu husika,Kila niandikapo juu ya kumsaidia msanii kuna baadhi ya watu wamekuwa wakiniuliza maswali ambayo ni tata ila si semi wamekosea hapana ila unapouliza kwanii wasanii hawatoshi kumchangia nataka ufahamu kuwa swala la kumsaidia mtu halichagui ni sawe na wewe mdau upate ajali kisha watu waje waseme kwani wafanyakazi wenzake hawatoshi mpaka sisi tumbebe kumpeleka hosptali kwa kweli haipendezi kama umeona huwezi au hukujaliwa waache wenye nacho na moyo wakutowa wamsaidie.
The super stars tz  itaendelea kuwaletea za ugonjwa wa matumaini kwa ukaribu zaidi na maendeleo yake, mungu atambariki dada yetu atapona kwa uwezo wake mungu.

No comments:

Post a Comment