Monday, January 28, 2013

HALI YA MZEE SMALL WANGAMBA NI MBAYA WADAU MPO WAPI..

Hapa alipokuwa mzima haumwi
Wadau nalazimika kuandika habari hii huku machozi yakinilenga kwa jinsi nilivyofanikiwa kuona hali ya msanii mahiri wa maigizo ya vichekesho nchi mzee wetu small ambaye kwa sasa hali yake inazidi kuwa mbaya kiukweli anatia huruma mzee wetu


Nadhani mtakubaliana na mimi kuwa page yetu ambayo ni page pacha na blog hii ya the super stars iliwahi kuandika kuhusu hali ya mzee wetu na kuwataka wasanii na wadau wenye mapenzi mema na mzee wetu kufika kumuona na kumjulia hali kwani hali yake sio nzuri

Sasa leo na kuja tena mbele yenu huku nikiwa nimepiga magoti chini kwakuwa nimeishuhudia hali ya mzee wetu kwa macho kiukweli wasanii mmemsahau mzee wenu na hata wapenzi pia mmemsahau mzee small ambaye alikuwa anakuburudisha na kukufanya ufurahi kila ulipoangalia kazi zake.
Hapa wakati yupo hosptalini

Kusema mmemsahau sina maana kuwa hamjishughulishi nae hapana ila kwa niwajuavyo mimi kiwango mnachokionyesha kwa mzee wetu nikidogo sana ukilinganisha na hadhi na ukaribu wa mzee small kwenu.
 kusema kweli ni aibu lakini ni bora kusema hata nikichukiwa nitakuwa nimesema mzee small anaumwa sana na hali yake ni mbaya pia anahitaji msaada wa hali na mali ili aweze kupata huduma,

Kiukweli naweza sema niwashukuru sana  TAFF kwa kuonyesha kujali kwani juzi baada ya tamasha la usiku wa mastaa Raisi wa shirikisho la wa sanii nchini tanzania alitowa shilingi laki moja na kukabidhi kwa mwenyekiti wake kwa ajili ya kuipeleka kwa mzee wetu huyo,Akizungumza na sisi muda mfupi uliopita Raisi wa shirikisho la filamu nchini bwana Saimon mwakifwamba amesema kuwa ,,Sisi bado tupo paamoja na mzee wetu na hata pesa zilizopatikana juzi katika tamasha la usiku wa mastaa nimempa mwenyekiti laki moja apeleke kwa mzee wetu ili imsaidie kwanza wakati tunaandaa njia mbadala kwaajili ya kumsaidia mzee wetu alisema mwakifwamba.

Hapa akiwa na man na bi chau
Mzee small anasumbuliwa na ugonjwa wa kupooza na  pale hali yake inapokuwa kidogo afadhali  anapelekwa muhimbili kwa ajili ya mazoezi
Tulipata nafasi ya kuongea na kiongozi wa kundi la bongo movie unt Ndugu Vicent kigosi ama Ray naye kwa upande wake alisema tumejipanga katika hilo na hata pesa iliyotoka juzi ni mipango ya pamoja  na kuongeza kuwa wao wamejipanga kufanya jambo kwa ajili ya mzee wetu huyo na kusisitiza watakaa kikao na raisi wawasanii nchini bwana mwakifwamba kuona ninamna gani watalifanikisha hilo

Najua kutowa ni moyo lakini kiukweli ifike wakati tujue pakuweka neno hilo kwani naamini kama tukiamua inawezekana kwa mzee wetu naamini kwa siku magari yenu yanatumia zaidi ya laki na simu zaidi ya hamsini na manywaji zaidi ya laki tano sasa ombi letu the super stars hebu jifungeni kwa siku moja na muweke kamchango muone mtakavyopata pesa nyingi zitakazo saidia kumtibu mzee wetu na kumpatia chakula.

Nataka tuamini kuumwa au kufa kwetu ni kama cheni leo yeye anaumwa kesho wewe sasa angalia hao unaowaona marafiki leo ujue watakukimbia kesho kama walivyomkimbia mzee small leo maana nachojua pia mzee wetu kabla ya kuumwa alikuwa na marafiki wengi sana wengine ni mastar leo waliofika kwake enzi hizo wakimuomba awasaidie kuingia katika maigizo lakini leo wamemtosa sasa kwanini washindwe kwako,hebu tujitowe sasa tusisubiri hadi mtu adondoke ndio tuanze kwenda na magari ya kifahari na kuandika katika page zenu tulimpenda sana mungu kampenda zaidi unafki mtupu mbona hamuonyeshi huo upendo leo.

The super stars ipo pamoja na familia ya mzee wetu na ina muombea mungu mzee wetu small ili apone na arudi katika hali yake ya kawaida kama zamani.tunaamini kwa uwezo wa mungu mzee wetu atapata nguvu tena kwani mungu hashindwi na kitu.

No comments:

Post a Comment