Saturday, January 26, 2013

HAWA NDIO WASANII WALIOKIMBIZA SOKONI 2012 KANUMBA LULU WAWA GUMZOMAREHEMU STEVEN KANUMBA THE GREAT

The super stars ikishirikiana na mitandao miingine ya kijamii ilifanya tasmini na kukusanya maoni ya wadau wa filamu kuhusu wasanii 15 wa filamu waliongaa mwaka 2012 Ilitulazimu kuchuku muda kidogo kwetu kutowa tasmini  kwasababu tulifanya tasmini ya ndani sana na tukazunguka hadi mikoani kwa ajili ya kukuletea tathimini yenye uhakika toka kwa wananchi.

 Na ikumbukwe kuwa maoni haya ni ya wenye maduka ya kuuza cd jumla na rejareja na kwa wale wakodishaji  bila kusahau wanaotembeza mitaani yaani machinga .

Hizi ndizo nchi na mikowa tuliyotembelea

Mwanza,Arusha,kilimanjaro,Tanga,morogoro,mbeya,dodoma,iringa,Na mwisho tulimalizia daresalam na haya ndio majina yaliyopendekezwa sana.

Kwa upande wa nchi Ni pamoja na kenya,burundi,rwanda,congo, Naomba ieleweke hii ni kwa mujibu wa mashabiki wenyewe madukani na the super stars imejifunza unaweza kupendwa sana mtaani ila wanakupenda sio wanunuzi wa kazi zako ila ni mashabiki tu sasa maaoni tuliyokuwa tunakusanya sio nani anapendwa zaidi ni nani anauza zaidi mtaani na maoni ya maduka ya kanda ni hayo hapo chini


Marehemu Steven kanumba
(1). Steven kanumba...Huyu jamaa pamoja na kwamba mwenyezi mungu ameshamtanguliza mbele ya haki lakini bado kwa sokon ni balaa hadi sasa anavunja rekodi ya mauzo kwani kila duka tuliloingia kuongea nao walisema ukiweka kanda ya marehemu haikai hata dakika moja, tena watu wanataka hadi ile michezo yake ya zamani iwekwe kwenye cd walisema wenye maduka ya kanda ambao ndio wauzaji wakubwa wa filamu hizo


Msanii Vicent Kigosi ,,Ray
(2). Vicent kigosi Ray...Huyu jamaa anatajwa kuwa ndiye msanii wa kwanza wa filamu anayeongoza mkwanja mrefu, watu haswa kongo rwanda burundi na hapa bongo huyu jamaa amechukua nafasi ya juu sana katika mauzo na wananchi wanasema wao wanampenda jamaa kwa kuwa ni msanii wa kwanza tanzania anayetengeneza filamu zenye hali nzuri yaani Quality ya kutizamika kuliko msanii yeyote hapa bongo na kwa hili hata marehemu au jb wote wanakiri kuwa kwa picha ray ni kiboko pia msanii wa kwanza wa filamu anyemiliki kampuni kubwa na yenye vifaa vya kisasa na vingi vya kushuti filamu hilo halina ubishi hata kwa wasanii wenyewe

Msanii Jacob Stephan,,Jb
(3). Jacob stephan Jb,,,,Huyu mara nyingi hupenda kuitwa bonge la bwana jamaa anafanya vizuri sana katika kiwanda cha movie bongo na anasemekana ni kati ya wasanii walio na mashabiki wengi haswa watu wazima ambao wao hunua sana filamu zake kwaajili ya watoto kwakuamini huwa jamaa hatengenezi picha za watu kuvaa nusu uchi japo tulishaona filamu zake kadhaa za wanawake kuvaa hivyo

Msanii Iren Uwoya
(6). Iren Uwoya ,,,,,Mwana Mama huyu wa mtoto mmoja alikimbiza sana dukani na bado yupo sokoni na ni kati ya wanawake waliofanya filamu zetu kuitwa filamu za oprah huko nnje wakimaanisha filamu za bongo Uwoya anafanya poa sana ndani na nje ya nchi hii na kwa mwaka huu alihojiwa na mtandao huu akaeleza kuwa yupo mbio kwenda uingereza kwa ajili ya kushuti filamu huko

Msanii Jackline Wolper
(7). Jacline wolper masawe,,,Huyu yeye kwa taarifa za mwaka huu kutoka kwa msanii mkubwa ambaye anategemea kufanya nae kazi anadai wahindi wanasema ni kati ya wanawake wanaouza kwa sasa na kwa upande wa huko mikoani mashabiki wanamkubali sana na anatajwa kuwa ndio mwanadada anayeongoza kwa mkwanja mrefu kwa sasa katika tasinia ya filamu.

Msanii Elizabeth Michaell,,Lulu
(8). Elizabeth Michael ,,Lulu,,,Huyu toka alipohusishwa na kifo cha marehemu kanumba basi hadi leo amejikuta akifanya vizuri sana hasa nchi za nje kama congo,Burundi,kigali rwanda,kenya,na huko mikoani,lulu amejikuta akifanya vizuri kwakuwa wengi wao walitaka kumuona na kumjua mtu aliyesababisha kifo cha kipenzi wao marehemu kanumba hivyo kujikuta lulu akiuza sana cd alizocheza.

Msanii Singo Mtambalike.. Rich Rich
 (9). Singo Mtambalike Rich Rich,,huyu jamaa amejikuta akikusananya mashabiki wengi sana toka enzi zile za swahiba na mahabubu mashabiki wanasema rich hakosei na ana aminika kwa utunzi wa story nzuri na pia ni mtu ambaye hapendi kuita filamu zake majina ya kizungu rich ni kati ya wasanii wanaokimbiza sokoni.

Msanii Wema Sepetu
(10). Wema isack Sepetu,,,Huyu yeye alianzia kupata umaarufu wakati wa mashindano ya miss tanzania na kuwa mshindi na hapo ndipo marehemu kanumba alipokiona kipaji chake na kumtambulisha katika filamu,japo mwana dada huyu hajaonekana katika filamu kwa kipindi kirefu sasa ila bado anauliziwa sana sokoni hasa movie yake iliyotumia gharama kubwa na kufanyika uzinduzi wa gharama uliomleta mwadada nyota ndani ya Nollywood Omotola jalayde kwa sasa wema ndio mwanamke ndani ya tasnia anayemiliki gari ya kifahari Aud Q7 nyeusi

Msanii Aunt Ezekieli
(12). Aunt Ezekieli,,Huyu yeye alitikisa sana katika filamu zake na kufanya mashabiki kumuulizia baada ya kona ka kaa kimya Aunt kwa sasa ni mke wa mtu na kwa taarifa yupo mbioni kuondoka kwenda kwa mume wake Dubai.

Msanii Hissani Muya ,,Tino
(13). Hissan Muya Tino,,,,Huyu jamaa kwa sasa hashikiki kwa movie za Action kwani ametokea kuzimudu sana na kufanya vizuri ,Movie za tino zimejikuta zinapata mashabiki haswa wale wanaolalamika kuwa bongo watu wamezidisha mapenzi na kumfanya tino apate mashabiki wengi na kuongeza mauzo sokoni  nadhani utakubaliana na kama utakuwa umeiona CID filamu iliyochezwa katika kiwango cha kimataifa

Msanii Ivin Shery,,Monalisa
(14). Ivone Shery,,,Monalisa,,Mwanadada huyu ni kati ya wadada wenye ndoto ya soko la nje zaidi nadhani ndio mana hata haonekani sana katika filamu zetu na dhani utakubaliana na mimi mwa jana wote monalisa alikuwa nchini gana kwenye kujaribu kushiriki filamu na mastar wa ulaya na alifanikiwa kupita yeye na marehemu kanumba ila baada ya kanumba kufa hatuelewi tena chochote maana yeye alikuwa mwepesi wa kutupa habari,,Tunaomba mona kama utakuwa unalolote kuhusu ile inshu ya ghana tujulishe na sisi tuwajulishe mashabiki zako wanaotaka kukujua
Msanii Anifa Daudi ,,Jenifa

 (15). Jenifa Daudi ,,Janifa,,,,Huyu nadhani ndiye msanii mtoto mwenye mafanikio katika sanaa ya bongo movie.jina la janifa lilikuja kwa kasi baada ya marehemu kanumba kumvumbua na kumchezesha katika filamu zake kama This is it na Uncle JJ ambazo alifanya vizuri hadi kufikia congo watu kumuita malikia wa watoto wa bongongo movie nadhani mtakumbuka janifa hakuwa katika orodha ya wale wasanii waliotakiwa congo ila baada ya kupeleka mabango yao kule kongo mashabiki waliyarudisha na kusema lazima jenifa aende jambo lilifanya watu wampeleke na kufanya shangwe kwa mashabiki wake.kwa sasa jenifa anatamba na filamu ya maduhu aliyocheeshwa na capturado


Hayo ndio maoni ya wauza maduka ya kanda pamoja na wanaokodisha kwa upande wa mwaka jana ila wadau nimejifunza kitu ambacho sikuwa nacho kumbe unaweza kuwa na mashabiki wengi sana ila wakawa sio wanunuzi wa kazi zako na unaweza kuwa na mashabiki wachache ila ni wanunuzi jambo ambalo kuna baadhi ya watu hapa mitaani kila siku mashabikia wanabishana na kuonyesha kuwa wapo juu ila ukija kwenye maduka kazi zao zimedoda kiukweli ziara yetu imetufunza mengi sana

Tunachowashauri wadau hakikisheni kama mnampenda mtu onyesheni kwa kumuunga mkono kazi zake ndio utakuwa umemfanya kweli awe juu badala ya kumshabikia tu na mwishowe anakuwa maskini na yule mnayesema hafanyi kitu ndio anasonga.....Hili  ni wazo letu tu  wadau.

No comments:

Post a Comment