Saturday, January 26, 2013

HUYU NDIYO YULE MBUNGE SHAROBARO NA MWENYE VITUKO HUKO KENYA

Huyu ndiye mbunge kijana rafiki wawasanii nchini kenya Mike Sonko
Kama utakuwa mfuatiliaji utakubaliana na mimi kuwa sonko ni mbunge kijana anayependwa nchini kenya ila pia ni mbunge asiyeisha vituko na ndio maana haishi kuandikwa na vyombo vya habari kila kukicha.

Mbunge huyo anaongoza kwa kupiga pamba huku akiwa ni shabiki mkubwa wa muziki na wanamuziki wa kizazi kipya.

Umeona mambo hayo
Hichi ndicho kiduku alichoingia nacho bungeni
Kama utakumbuka aliwahi kutinga bungeni akiwa kavalia suti nzuri ila kavaa hereni jambo lililomfanya spika wa bunge la kenya kumtowa nnje ya bunge kwa kuvunja kanuni za bunge.na hivi karibuni page yetu ya the super stars iiliripoti na kuonyesha picha za mbunge huyo alipotinga bungeni huku akiwa kanyowa kiduku na kukiandea Peace 
.
Huyu ndiye sonko mbunge shararobaro
Sonko kwa sasa ni kipenzi cha wasanii wa kenya kwani wanadai anawajali na kuwasemea sana bungeni na wanaamini kuwa ndio mtu pekee anayejuwa matatizo yao kilisema chanzo cha habari hii kutoka nchini kenya.
Mbunge huyu ambaye ukikutana nae mtaani huwezi jua kama ni muheshimiwa kwa jinsi alivyotupia kisharo aliwahi kusema kuwa kuwa vile alivyo ni maisha yake na hadhani kama anapaswa kuingilia na mtu yeyote.

Msanii kutoka tanzania Z Anto Ni kati ya wa sanii wa afrika mashariki waliopata baahati ya kukutana na mbunge huyu na kujikuta akipewa gari la kifahari sana na walinzi lukuki kwaajili ya kuzunguka nae mitaa yote aliyotaka nchini kenya.
Aliwahi pia kuripotiwa na vyombo vya habari kuwa ni kati ya wabunge vijana wenye mafanikio makubwa na pia ni kati ya wabunge wanaotetea na kuupenda muziki wa nchini kenya.

No comments:

Post a Comment