Sunday, January 27, 2013

JOSE CHAMILIONE MSANII BILIONER NA ANAYEMILIKI NYUMBA ULAYA


Huyu ndio Dk.Jose Mayenja ChamilioneNajua unajiuliza kwa nini ninamwita Bilionea!nina haki kumuita bilionea msanii huyu kutokana na mali alizo,msanii huyu amekuwa ni kipenzi cha waganda kutokana na utunzi wake na sauti aliyonayo iliyofanya hata hapa tanzani tumpende sana nadhani utakubaliana na mimi kuwa ni msanii wa afrika mashariki mwenye mashabiki wengi anapokuja hapa nchini.


Msanii huyu wa uganda ni mmoja kati ya wasanii matajiri afrika Anamiliki jumba la kifahari katika vilima vya Sekuku jijini Kampala, pia ana nyumba huko Arizona, Marekani, achilia ile ya Kigali, Rwanda aliyoinunua hivi karibuni kwa mamilioni ya shilingi.,pia ana miliki mjengo wa maana katika ufukwe wa ziwa victoria kwa upande wa tanzania akiachilia mbali nyumba zake za kuishi jamaa ana miliki hoteli na apatment nyingi sana ndani na nje ya nchi pia msanii huyu anamiliki magari ya kifahari sana na ya garama kubwa tatu ana miliki mradi wake wa simu unaitwa chamilion phone  

Hapa chini ni Baadhi ya majengo  na magari yake...


JUMBA LA CHAMILIONE
Hii ndio nyumba Chamilione aliyomnunulia mkewe na kumpa zawadi
Mjengo wa chamilioni uliohusishwa na kijana kujichoma moto hapa polisi walipokuja kufanya uchunguzi
GARI AINA YA ESCALADE MALI YA CHAMILIONE LIKIWA LIMEPAKI NYUMBANI KWAKE

Ukiachilia mbali gari la kisasa aina ya Cadillac Escalade lililomgharimu zaidi ya Sh milioni 100, Chameleone ambaye ni baba wa watoto watu, pia anamiliki Mercedes Benz, BMW RANGE,VOGUE na aina nyingine za magari.
Chamilione akiwa amepozi kwenye moja ya gari lake


Jose Chamilion Katika gari yake nyingine


GARI LA JOSE AKIWA AMEANDIKA JINA LAKE
MAGARI YAKE YOTE YANATUMIA NAMBA ZA MAJINA YAKE

 
Kwa ujumla, anakadiriwa kuwa na utajiri unaofikia Sh bilioni 1.8 kwasasa kwa fedha za Tanzania. Na anasema bado hajaridhika kwani ataka kurudishia jamii yake shukrani kwa kuwatengenezea vitu kibao ikiwemo kituo cha kuwasaidia wazee na nwatoto ya tima..
Jose chamilion anasema muda mfupi ujao atamiliki ndege yakemwenyewe
CHAMILIONE AKIWA HOLLYWOOD MAREKANI NA HAPA AKIWA KAPIGA PICHA NA SANUMU LA MAREHEMU  MICHAEL JAKSON
Mke wa chamilione Daniela Atim akiwa na familia yao nnje ya nchi

Msanii huyo anamiliki mkwanja mrefu sana katika akaunti yake ukiacha majumba ya kuishi msanii huyu ana miliki jumba jingine la kifahari ufukweni mwa ziwa victoria kwa upande wa uganda,pia ana apartments kibao huko uganda.


Msanii huyo wa kimataifa anasema yeye alikuwa ni mtu maskini sana ila akaja kutolewa na mwanamke aliyemtaja kwa jina moja la Dorothea ambaye alimpa milion moja na nusu na kumfadhili kukaa kwake kipindi hicho jose analala studio.anasema chamilione

Nilipohamia tulikuwa marafiki, lakini mengine yaliibuka tukiwa katika nyumba moja. Mara nyingi kila akitoka, alinikuta nimetulia naandika nyimbo zangu huku akihoji ni lini nitarekodi. Nilikosa jibu kwa kuwa sikua na pesa za kuingia studi kwa wakati ule


Chamilione na mkewe wa sasa siku ya ndowa yao
Siku moja alisafiri na bila kuniaga na kuniachia katika bahasha dola 1000 ambazo ni sawa na shilingi milioni 1.5 na kitu kwa pesa za kitanzania
Huo ukawa mwanzo wa kibao Mama Mia na sikuamini kama fedha ile ingebadilisha maisha yangu na kunifikisha hapa nilipo. Mengine yanabaki kuwa historia,” anasema. 

Pamoja na utajiri aliovuna kupitia muziki, nyota huyo anasema historia ya kushuhudiwa `Live’ na watu zaidi ya bilioni 9 akitumbuiza wakati wa Kombe la Dunia kwake ni kitu cha kipeke sana na anaona ni zaidi ya hata utajiri alio nao.
 Haya wasanii wetu wa hapa nyumbani tujipange nadhani kwa maelezo ya Dk Jose Chamilione kama waganda wanavyomuita alivyoeleza kuwa alikuwa na maisha ya shida na hata pakulala pia alikuwa hana ila kajikuta ni bilioner huu ni uwezo wa mungu na ukitia bidii naamini muna weza anzeni sasa kujituma na muache kulewa sifa. 

No comments:

Post a Comment