Tuesday, January 29, 2013

LULU AACHIWA RASMI BAADA YA DHAMANA YAKE KUKAMILIKA ..ANGALIA JINSI VILIO VILIVYOTAWALA DK CHENI AWA NA KAZI YA KUTULIZA


Lulu na mama yake mzazi wakilia baada ya kukutana nje ya Mahakama, Lulu amechiwa huru na Mahakama leo january 29 2013 mchana, pembeni ni mwigizaji Dr. Cheni ambae amekua karibu na familia ya Lulu kwa muda mrefu sana.

Ama kwa hakika nnje ya mahaka pamegeuka kilio mara muigizaji elizabeth michael kuachiwa kwa dhamana leo tarehe 29 lulu amepewa dhama kutokana na kesi inayomkabili ya kumuuwa bila kukusudia aliyekuwa star wa bongo movie marehemu steven kanumba.

Mara baada ya lulu kumuona mama yake wamejikuta wakiangua kilio hadi watu wakaribu wakawa wanashangaa.kazi ilikuwa kwa muigizaji dk cheni ambaye kiukweli katika watu wakupongezwa katika hili anachukuwa nafasi ya kwanza kwa binadamu ,cheni amekuwa mstari wa mbele kumsimamia lulu hadi amepata dhamana.

Lulu akiingia kwenye gari huku akisaidiwa na Dk cheni kwa nyuma yake
Mama yake lulu aliwahi kukaririwa akisema kwa sasa anamuona cheni ni zaidi ya binadamu wa kawaida kwani bila yeye hajui kama ataweza kumuokowa mwanae mama huyo amejikuta akilia kwa furaha baada ya kumuona tena mwanae huyo.

Dk chen amezungumza na thesuperstarstz na kutuambia anashukuru mungu kwakumpa moyo wa ujasiri wa kumsaidia binti huyo kwani wengi walimsusa lakini tukumbuke mungu ndiye mlipaji wa yote hatupaswi kumuhukumu mtu kwani hata mahakama bado haijamuhukumu lulu sasa sikuona sababu ya baadhi ya wasanii kujitenga na lulu na ndio maana nikajitolea kumsaidia hadi nijue mwisho wake.

Lulu akilia kwa furaha na kushindwa hata kuongea chochote alipokuwa anahojiwa jambo lililofanya cheni amuongelee
Cheni ambaye ni mmoja kati ya wadhamini waliotowa milioni ishiri 20 za kitanzania cheni amekuwa masaada mkubwa sana kwa lulu jamba ambalo limefanya lulu kumuona cheni ni zaidi ya baba yake kwa sasa na ndio maana mara nyingi hata kabla ya tukio la lulu na kanumba kutokea  bado lulu alikuwa anamuita cheni baba japo  haikujulikana kwanini na cheni katika familia ya kina lulu anaheshimika sana na ndio maana haikuwa rahisi kwake kutojitolea kwa hilo.

No comments:

Post a Comment