Monday, January 28, 2013

LULU AACHIWA HURU KWA DHAMANA...


Msanii lulu
Hatimaye yametimi leo kwa msanii elizabeth Michael kutokana na kesi yake mahakama kuu ya Tanzania imekubali  dhamana ya msanii wa filamu nchini Tanzania, Elizabeth Michael aka Lulu aliyekuwa mahabusu katika gereza la Segerea jijini Dar es Salaam, nakilichobaki ni hatua chache ili lulu awe uraiyani

Msanii Elizabeth Michaell

Kama utakuwa unakumbukumbu wiki iliyopita mawakili wa muigizaji huyo waliwasilisha maombi ya dhamana kwa mahakama hiyo kuu ya Tanzania.
Wanasheria hao Peter Kibatala, Kennedy Fungamtama na Fulgence Massawe waliomba dhamana hiyo itolewe haraka kwakuwa muombaji amekaa mahabusu kwa zaidi ya miezi saba na kwamba kosa lake linaweza kupewa dhamana.

 Pamoja na dhamana hiyo kukubaliwa  lakini bado msanii huyu maarufu kwa jina la lulu anakabiliwa na kesi ya kumuua bila kukusudia Steven Kanumba April 7, 2012, huko nymbani kwa marehemu Sinza Vatican, jijini Dar es Salaam.Kanumba alidaiwa kuwa kwenye ugomvi na Lulu aliyekuwa mpenzi wake nyumbani kwake Sinza vatcan jijini Dar es salaam.

No comments:

Post a Comment