Monday, January 28, 2013

LULU ARUDISHWA SEGEREA TENA BAADA TARATIBU ZA MAHAKAMA KUKWAMA

Msanii wa filamu nchini, Elizabeth Michael ‘Lulu’ akitoka katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, leo baada ya Msajili wa Mahakama Kuu kutokuwepo ofisini na hivyo kurudi rumande hadi kesho tarehe 29/1/2013 atakapoletwa kwa ajili ya kutimiza masharti ya dhaman. 


 Mahakama Kuu ya Tanzania leo  mchana  iliweka wazi masharti ya dhamana ya msanii  wa filamu anayejulikana zaidi kwa jina la Lulu,. ambaye jina lake halisi ni Elizabeth Michael.....
Gari lililomleta Lulu likiondoka mahakamani leo

Kwa mujibu wa chanzo chetu kilichokuwepo mahakamani mchana , dhamana ya mwigizaji Lulu ipo wazi endapo tu angetimiza masharti yaliyotengewa ambayo ni

  • Kuwasilisha au kukabidhi hati yake ya kusafiria(passport)
  • Kutosafiri nje ya Dar es salaam.
  • Kuripoti mahakamani kila siku ya kwanza ya kila mwezi
  • Kuwa na wadhamini wawili ambao kila mmoja atamdhamini kwa shilingi milioni 20 za kitanzania.
Pamoja na kwamba familia ya Lulu walikuwa wamejiandaa kukabiliana na kutimiza masharti hayo, Lulu amerudi rumande leo kutokana na kwamba  watumishi wawili wa serikali(Mahakama) ambao wanahusika na sehemu ya dhamana hiyo kwa upande wa sahihi za kimahakama, hawakuwepo Mahakamani hapo .....
Hata hivyo, kwa mujibu wa mawakili wanaomwakilisha Lulu, masharti yote ya dhamana wameshayatimiza na kinachosubiriwa ni huo uthibitisho na utaratibu wa kimahakama ili Lulu arejee nyumbani na kuendelea kukabiliana na kesi hiyo akiwa uraiani.
Gari aliloondoka nalo lulu leo
Kwa maana hiyo ni wazi kabisa kwamba Lulu atatoka kesho cheni amesema kuwa mambo yote yalikuwa sawa tatizo ni hao jamaa wawili ambao walitakiwa ku saini kutokufika hadi muda wa mahakama unaisha,mama wa lulu nae aliongeza kusema kuwa awali walikuwa wamemaliza kabisa na hata baadhi ya vyombo vya habari viandika kwa kwakujiamini kutokana na maneno yetu kwani tulishamaliza na hata jamaa hawakutowa taarifa za kutokuja sasa sijui tatizo nini ila mungu akipenda kesho lulu atatoka na tutakuwa nae alisema mama huyo wakati akimuangalia mwanae alivyokuwa anapanda gari la magereza tayari kwakurudishwa segerea.

No comments:

Post a Comment