Thursday, January 31, 2013

LULU FEKI ACHANGISHA PESA FECEBOOK HUKU AKITOWA AHADI KUWA WENYE VIPAJI WAFIKE KWAKE ,DIAMOND PLATNUM NA DOCTOR CHENI NAO WAMO

MSANII MAHSENI HAWADHI DK CHENI
Msanii wa filamu nchi na anayeaminika kuwa na mkwanja mrefu mahsen hawadh alimaarufu kwa jina la dokta cheni ameibuka na kulalamikia kitendo cha watu kutumia jina la msanii mwenzeka lulu katika facebook na kuomba pesa kwa watu,huku pia akiandika vitu ambavyoo lulu hausiki navyo

Cheni amesema jambo hilo si la kiungwana na nikama kufanya wizi kwa kukutumia jina la lulu,cheni ameendelea kutiririka kuwa amestushwa na watu wanaomjua kumpigia simu na kumuuliza kama kapata pesa walizomtumia na alipohoji za nini watu hao wakasema tumeambiwa lulu anataka mchango jambo lililomstua cheni na alipoelekezwa na kuingia ndipo nayee alijiona katajwa na kuwekewa namba feki kuwa ni ya kwake na mchango wa lulu utapitia kwake  huku lulu mwenyewe akiwa hajaomba na wala haitaji mchango wa pesa ,,cheni amesema kuwa yeye mwenyewe anauwezo wa kumsaidia lulu na kama kutakuwa najambo la kuchanga halitakuwa siri,,Mimi nadhani duwa za watanzania na na za wale waliombali na tanzania ila wanaipenda sanaaa yetu basi ni vizuri kumuombea lulu badala ya kutuma pesa duwa zenu ni muhimu sana kwa lulu hata nikiongea nae anasisitiza ni waombe mashabiki zake wamuombee duwa tu basi
PICHA YA LULU KABLA HAJAENDA JELA
Hili la kuomba pesa limeibuka masaa machache baada ya  lulu kupata dhamana kwani katika mitandao ya kijamii kuna watu wameibuka wakitumia jina la lulu michael,,,elizabeth michael,,,elizabeth lulu michael na lulu elizabeth michael kisha wameanzisha tabia ambayo imetafsiriwa na baadhi ya  wanasheria nakusema iwapo mtumiaji wa jina hilo na vielelezo vikaonyesha kuwa alilenga msaada huo upate kwa jina la mtu mwingine na akatumia vielelezo ambavyo vinamuhusu muhuska wa jina hilo  basi ni kosa ila kama alisema tu mumsaidie lulu bila kusema ni lulu yupi  bado sheria hambani ila hao wanautumia picha kisheria ni kosa alisema maliki mfinanga mwanaseria wa kujitegemea.

Watu hao wameandika na kuweka namba za simu huku akisema anahitaji mchango kwani amekaa gerezani hivyo hana kitu huku akiweka namba na kusema ni za doctor cheni kumbe ni uwongo mtupu,cheni amekanusha vikali swala hilo nakuwaomba watanzania na wadau wote kwa ujumla kuwa mtu asitume pesa yoyote kwa mtu yeyote kwani kwa sasa lulu hatumii kabisa mitandao ya kijamii kama fecebook,, tweet  na nyingine kwa hiyo hao wote ni lulu feki alisema cheni kisha akaendelea kuwa wao wanalifuatilia kwa umbakini na kwasababu namba aliyoweka itakuwa imesajiliwa basi sheria itachukua mkondo wake,

LULU AKILIA JUZI BAADA YA KUACHIWA HURU
Akiendelea kupiga story na the super stars tz cheni alisema kuwa lulu ameshangazwa sana na jambo hilo na anawaomba watanzania wazidi kumuombea duwa kama walivyofanya mwanzo na si pesa akizungumza na sisi kupitia simu ya cheni lulu alisema Mimi sipo fecebook jamani wala sitaingia fecebook kwa sasa hivyo nisaidie kuwaambia watu wote wajue hao ni lulu feki na wasitume pesa wala wasiwasikilize na mimi nipo kwenye matatizo lakini na shangaa kuona wanaandika eti  mimi nataka wasanii niwasaidie watoke kisanii kweli?alihoji lulu huku akilia kiukweli mdau inamuuma lulu kwani anahisi kama wanazidi kumpaka tope kwa jamii ambayo bado hajajisafisha kwao.

MSANII LULU KATIKA POZI
Watu hao wamefikia hatua leo kuandika hivi huku wakitowa namba ile ile ya voda pesa waliosema ni ya cheni sasa sijui  cheni kageuka kuwa meneja wa dimond au. lakini kama unavyojua blog yako hailali kwa ajili yako ilimuendea diamond haraka kutaka kujua ukweli wa hili ila hakupatikana na kumpigia rafiki wa karibu na msanii huyo nyota wa muziki wa kizazi kimpya ambaye alikanusha vikali na kusema kuwa rafiki yake huyo hana mpango wa chochote na wala hajafikia huko kwakugawa pesa naomba watu wajue alipoulizwa kama ameshamsikia dimamond akipanga juu ya hilo alisema kaka niamini mm nachokuambia hakuna hilo swala kama kugawa angeanza na sisi watu wake kama huamini subiri akimaliza kazi hapa nitakupa uongee nae.

Hii ni moja ya vitu alivyoviandika na hii ndio kaweka inamuhusu diamond

Je, wewe ni mwananchi mwenye maisha duni na ungependa ifikapo DECEMBER 31, 2013 uwe na mafanikio maishani mwako? kama jibu ni ndio, Diamond Platinumzz Beibi ameanzisha mfuko maalum kwa ajili yako, mfuko huu unatoa mikopo kwa mtanzania yeyote aliyefikisha umri wa miaka 18 na kuendelea, bila dhamana wala amana. pia awe na akili timamu. Masharti yake ni rahisi sana na yanaweza kutimizwa na mtu yeyote yule. Kwa mawasiliano zaidi piga simu namba 0767 231 685... NI WAKATI WAKO!!!

Onyo toka the superstars ni kwamba kwamujibu wa cheni ni kwamba ukimuona mtu yeyote anayetumia jina la lulu fecebook ujue ni faki na lulu mwenyewe ameahidi kuwa akiingia fb atawaambia mashabiki wake ila kwa sasa hatarajii hivyo epuka wizi na usitowe pesa kwani lulu hajasema chochote na hajaomba pesa yeye anaomba tu duwa zenu hivyo wadau tuungane kupinga jambo hili kwani ni kumchafua lulu.

LULU AKIWA NA ZAMARADI MKETEMA HUKU NYUMA YAO ANAOONEKANA MSANII THEA
Tamko rasmi ni kwamba lulu hayupo fecebook kwa sasa hao ni lulu feki na elizabeth michal feki chochote atakachoandika juweni si kwaajili ya lulu na si lulu ni mtu binafsi na mapenzi yake hivyo mnatakiwa kucoment kwakuwajulisha watu wajue sio lulu

Kwa hakika karibu wasanii wote wa muziki na filamu tuliowahoji wameonyesha kukerwa na jambo hili na kuwaomba mashabiki wao popote pale walipo wasitowe pesa zozote kwa mtu anayemtaja msanii kuwa anataka mchango huku wakiwaomba kila watakavyokuwa wanaona mtu anaandika habari za msanii haswa lulu ambaye yupo katika matatizo basi wa coment kwakumuumbua ili mtu mwingine naye asijikute kaingizwa mjini

No comments:

Post a Comment