Monday, January 28, 2013

SASA LULU YUPO URAIYANI RASMI

LULU ANAYETUHUMIWA KUMUUWA KANUMBA BILA KUKUSUDIA
Msanii elizabeth michel ameachiwa rasma na sasa yupo uraiyani lulu ambaye alionyesha kuifurahiya dhamana yake hiyo ameachiwa baada ya kuonekana kutimiza masharti yote waliyotakiwa kuyawakilisha ikiwa ni pamoja na hati ya ke ya kusafiria.

Lulu ambaye alikuwa mahabusu segerea toka april mwaka jana amejikuta akipew dhamana hiyo baada ya mawakili wake kuiomba na kufanikiwa kuipata leo hii,lulu ambaye muda mwingi alikuwa anakwepa camera ili asipigwe picha amechiwa huru ila kwa masharti ya kutokutoka nnje ya jiji la dar es salaam

MSANII LULU ALIYEHUSISHWA NA KIFO CHA KANUMBA
Kesi ya lulu inasimamiwa na mawakili wa nne ambao ni Peter Kibatala, Kennedy Fungamtama na Fulgence Massawe Ambao kwa pamoja wanasema wamfurahi sana mteja wao kupata dhamana ili kesi iongozwe akiwa nnje wakizungumza na sisi walisema kuwa lulu kwa sasa ni kama yupo huru tunasubiri kukabithi mashari tuliyopewa kwa wahusika wawili ambao inasemekana bado hawajafika hadi sasa
DK.CHENI MSANII ALIYEMSAIDIA LULU

Dk C heni ni kati ya watu ambao familia ya lulu inamuheshimu na kumuona kama mmoja wa familia toka zamani.cheni amijikuta akihangaika sana kuhakikisha lulu anapata dhamana na juhudi zake zimezaa matunda akizungumza na sisi msanii huyo asiyekuwa na wingi wa kashifa alisema kuwa hakuona sababu ya kutokumsaidia lulu maana mahaka ndio itakayo amua lakini mimi nafanya kwa uwezo wangu pale napoweza kumsaidia,cheni aliendelea kusema yeye anaamini kuwa kwa upande wake jambo hili limekuwa gumu sana haswa ukizingatia mimi na kanumba tulikuwa marafiki wakubwa sana na kwa upande wa lulu mimi wananichukulia kama mwanafamilia sasa nadhani utaona jinsi nilivyo na wakati mgumu ila wacha awe huru kisha mengi yatajulikana baadae alisema cheni ambaye alikuwa akisubiri jamaa wafike ili wawakilishe  mashariti waliopewa ili waruhusiwe kuondoka na lulu
MSANII LULU

Baadhi ya watu waliohudhuria mahakamani wamejikuta wakitokwa na machozi ya furaha mara walipoambiwa dhamana ya msanii lulu imekubaliwa,,,the super stars tz imeshuhudia tukio zima ,,,Ama kweli huyu mtoto anakubalika yaani watu wanalia bila kupigwa alisikika msukuma mkokoten mmoja akisema.Kwa upande wa mitandao ya kijamii lulu ameonekana kuwa na mashabiki wengi wanaosema bora awe huru na wengine wakishukuru kwa duwa kutoka kwake,kama utakuwa mtembeleaji mzuri wa facebook na tweet leo utakuta zimejaa pongezi kwa lulu na hata ukipita mitaani watu bado wametengeneza vikundi wakiongelea jambo la lulu.

The super stars tz  inamuombea atoke ila inawakumbusha wasanii na kumuomba tena cheni kuwa moyo aliouonyesha kwa lulu basi auonyeshe na kwa msanii kajala ambaye yupo gerezani kipindi kirefu sasa ili nayeye atoke kama lulu japo kwa dhamana kwani mashabiki wake wana mkumbuka sana
 Kwakumalizia thesuperstarstz inamshauri lulu kama atatoka basi atulize akili yake na kurudi kwa mola wake kipindi hichi wakati anasubiri kesi yake kutajwa.

No comments:

Post a Comment