Friday, January 25, 2013

MILIONI 20 ZAHITAJIKA ILI LULU MICHAEL AWEZE KUPATA DHAMANA HAPO KESHO


Yule mwigizaji nyota wa filamu za kibongo Elizabeth michaell huenda kesho akatoka kwa dhamana kama mambo yatakaa sawa Kwa habari za uhakika kutoka kwa chanzo makini kisichokuwa na shaka kimesema kuwa kuna uwezekano mkubwa kuwa muigizaji huyo mwenye mashabiki wengi ndani na nje ya bongo akatoka kwa dhamana kesho january 25 2013.

 Lulu ilibidi apate dhamana toka jana jumatano january 23 lakini ilishindikana ikabidi  hivyo kwasababu na kuahirishwa kwa sababu jaji alipata dharura na pia kiwango cha pesa za dhamana kilikua hakijatimia.

Chanzo cha kuaminika kilichoongea na millardayo kimesema dhamana ya kumtoa Lulu ambae amekua chini ya ulinzi kuanzia April 2012 ni milioni 20 za kitanzania.

Lulu amekua akishikiliwa kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya mwigizaji Steven Kanumba.....

No comments:

Post a Comment