Sunday, January 27, 2013

MTWARA NA MASASI ZA GEUKA UWANJA WA VITA

Jengo likiteketea moto katika vurugu hizo
Hali si nzuri huko mtwara kwa kile kinachodaiwa ni kugomea gesi asilia inayochimbwa katika eneo la msimbati mkoani humo,mabomu ya machozi na risasa zimetumika kuwatawanya wananch walikuwa wakiharibu na kutekeza mali za serekali

Nyaraka za serekali zikiteketea moto
Badhi za nyumba zilizochomwa ipo pia nyumba ya mkuchika akizungumza na blog hii mwananchi mmoja alisema kuwa maamuzi yao ni kwamba wapotiyari kufa ili kulinda gesi hiyo ambayo wanaamini ni raslimali ya watoto wao,akipga stor na sisi mwananch huyo alisema kuwa wamefikia mamuzi hayo kwakuwa serekali imewasahau sana na sasa wao wameamua kujitetea wenyewe na wanaamini kuwa watashinda kwa nguvu ya mungu.

Kama utakumbuka habari ya yule bibi aliyemuambia raisi jakaya mrisho kikwete kuwa gesi ile ikiondolewa kwa nguvu basi itakapofika dar itageuka maji kwa habari za uhakika ni kwamba wananch wanamlinda kama raisi.

Baadhi ya gari za serekali zikiteketea moto
Kwa taarifa za kuaminika toka katika familia ya bibi huyo na wananchi wengine ni kwamba majira ya saa saa 2 usiku walimuona mtu wanayemjua kwakuwa kazaliwa pale kijijini japo kwa sasa yupo usalama wa taifa( jina kapuni)akiwa na shangazi yake  walikwenda nyumbani kwa Bibi Mtiti wakiwa na gari mark 11

“Unajua yule bibi tunamlinda, sasa ilipoonekana ile gari usiku pale, watu wakaanza kujiuliza linafanya nini…wakaanza kusogea, kadiri muda ulivyokuwa unakwenda ndivyo watu walivyozidi kuongezeka,”alisema Juma Ayoub mkazi wa kijiji hicho.


Asha Hamisi ni mtoto wa pili wa Bibi Mtiti, akihadithia juu ya tukio hilo, alisema yapata saa 2 usiku wakiwa wanakula chakula walipokea wageni wawili ambao baada ya kumaliza kula waliomba kuongea na mkuu huyo wa kaya.


“Alikuja kijana na mama wakaniomba kuongea na bibi…alimuuliza bibi kama ana uwezo wa kwenda Mtwara, bibi akajibu hawezi…wakaniuliza mimi kama naweza kwenda badala yake nikawaambia siwezi…akasema ametumwa na Rais Jakaya Kikwete na Hawa Ghasia...wamjie bibi wakazungumze naye mambo ya gesi,” alisema Hamis.

Ndio hali halisi ya mtwara

Aliongeza kuwa “Kama bibi yupo tayari Jumanne ijayo watamfuata kwa gari…mimi nikasema sitaki…nilipochungulia nje nikaona watu wengi wamezunguka.”


Kwa upande wa mtoto mwingine wa bibi huyo alisema,” Kwa kuwa tunamfahamu tulimwambia aondoke mpango aliojia haufai, akawa anabisha, tukaendelea kumsihi..wakati huo watu wanazidi kuongezeka…alipotoka akakosea njia, alipopita hakukuwa na njia…watu walimfuata wakaanza kumrushia mawe…aliacha gari akakimbia…ndipo wananchi walipoliteketeza gari kwa moto,” alisema Manzi Mohamedi Faki mtoto wa tano wa Bibi Mtiti.
 

Walifikia hatua ya kubomoa hadi majengo ya serekali
Wakati huo huo watu watatu wamefariki dunia Mkoani humo baada ya vurugu hizo  kati ya Askari wa Jeshi la Polisi na waendesha Pikipiki maarufu  (Bodaboda).

Ndivyo gari hii ilivyoteketezwa na wananchi hao wenye hasira

Wakati huohuo kuna taarifa kutoka Masasi zikieleza nako kuibuka tukio la chomachoma mchana huu wa leo ikihusisha uchomwaji wa Offisi za Serikali, Polisi, nyumba za Wabunge na Offisi za CCM. Hali ya Masasi inaelezwa kuwa ni tete zaidi kuliko ilivyokuwa hapa Mtwara Mjini usiku wa jana ingawaje napo palikuwa na kimuhemuhe cha mabomu ya machozi kutoka kwa polisi.

Bado mpaka sasa haileweki ni nini hasa hatma ya mgogoro huu, maana kwa upande wake Serikali inaonekana kushikilia msimamo wake uleule wa kutaka kusafirisha gesi hiyo wakati upande wa raia wakiwa na msimao wao wa GESI KWANZA MAISHA BAADAYE, kwa maana kutoridhia usafirishaji wa gesi hiyo ikiwa ghafi kupelekwa Dar es salaam


Wito  kwa Serikali ni kwamba ikae na wananchi ili kujadiliana juu ya mstakabali mzima wa tatizo hili na kutafuta suluhu. Muda ni huu kwa sababu si vyema kuacha hali iendelee kuharibika ndipo tuje baadaye tulazimike kuunda tume za watu kuchunguzwa. Si vibaya kwa Serikali kukiri au kurudi kwa raia na kusema pale ilipoteleza na kutafuta ni namna gani na ni njia ipi sahihi ya kuliendea suala hili.

  Haya mungu ibariki tanzania yetu

No comments:

Post a Comment