Friday, January 25, 2013

TUMECHOKA KUUWAWA, KUBAKWA NA KULAWITIWA SEREKALI MKO WAPI?Polisi wakiwa katika doria kuhakikisha usalama unakuwepo
Ama kwa hakika wanafunzi hawa wa st john's walionyesha kuchoka na hali ile ni majonzi matupu

Hii ndio ilikuwa hali  halisi kwa wanafunzi wa st .john's
Barabara zilisitisha shughuli za kupita magari kwa muda kutokana na wingi wawanafunzi hao

Kama kawaida ya maandamano mabango yalitawala
Walizidi kumiminika
Polisi walifika na maji ya kuwasha lakini haikuwasaidia kwani wanafunzi hawa kwani walishajawa na moyo wa chuma kutokana ma matukio ya ubakaji na mauwaji yaliyofanyika kwa mwanafunzi mwenzao


Mdau hii ndio jamii iliyochoka kwa ubakwaji

Mabango yenyewe yalikuwa ni njia tosha kusema ya moyoni

Polisi walitanda kila kona
Haikuwa rahisi kuwadhiti wanafunzi hawa

Bado walizidi kujaa hata wananchi wa kawaida walioguswa nao hawakuwa nyuma
Polisi wakihakikisha usalama
Nadhani mdau unaona umati ulivyofurika kupinga ubakaji kwa wanafunzi na mauwaji
Polisi walikuwa na kazi kubwa
Hii kali mpaka trafk walidandia magari badala ya kuyaongoza magari
Hapa ndipo safari ya maandamano ilipoanzia na ndipo safari hiyo ilipoishia maeneo haya ya kwenye bendera mbele ya jengo la administration.
Baada ya kumaliza maandamano

Baada ya wanafunzi hawa wa chuo cha st.john's kuhakikisha kuwa safari yao ya maandamano ya amani imekamilika wanafunzi hao walijipumzisha katika miti kadhaa iliyokuwepo chuoni hapo,maandamano hayo yalikuwa yanahusu kupinga mauwaji yaliyotokea chuoni hapo yakimuhusisha  mwanafunzi mwenzao lidya leo pia wanafunzi hao walikuwa wanapinga maswala ya ubakaji na kulawitiwa na watu waliowaita vibaka ambao huvamia chuoni hapo na kuiba laptop simu pesa na vitu vingine vya dhamani kisha kuwabaka na kuwalawiti wanaume ili kuonnyesha kuchoshwa na mambo yale jana hiyo hiyo asubuhi majira ya kumi na mbili alfajiri kuna wezi waliingia na kuiba laptop na baada ya wanafunzi kuzisikia walikusanyana na kumsaka mwizi wao walipompata walipiga nusu ya kumuuwa nandipo polisi walipofika  na kumuokowa kisha kumpeleka kituoni

No comments:

Post a Comment