Tuesday, January 22, 2013

RAY AANDAMWA KUHUSU FILAMU YAKE..... WADAU WAHOJI BODI YA FILAMU IMELALA AU IMEAKUFA.?


Wadau najiuliza kwanii watu wameamua kumuhukumu ray kabla hata filamu yenyewe haijatoka na kama ray kakosea inapaswa bodi ya filamu ilione hilo na kulikemea sio mpaka waandishi wahabari waone wajadili waandike nyie mpo wapi.

Moja ya magezet yaliyomuandika ray
Nachokijua mimi ni kuwa bodi ya filamu kazi yake ni kudhibiyi filamu zilizokiuka maadili sasa filamu kama sister mary ya ray ambayo inazungumziwa sana kuwa imedhalilisha ukristo na kuwa inasukwa njama ya kumuuwa ray sasa hebu tujiulize kama ni kweli inamaadili mabaya mbona hao bodi ya filamu hawakusema mapema na waliiona promo zake zaidi ya miezi mitatu ina maanisha kazi ya bodi ya filamu hapa nchini ni swala la kuyategemea magazeti inamaana magazeti yasipoandika hata kama kitu ni kibaya basi mtakiacha sasabubu hakijaandikwa.

Blog hii imefanikiwa kuongea na mashabiki wa filamu maeneo ya kariakoo katika maduka ya kanda ambapo wadau hao walionyesha kuwa wanaisubiri kwa hamu na kila mtu alisema kuwa ilibidi filamu ikaguliwe kabla hata ya kuirusha promo sasa umesharusha promo ndio unaifungia filamu inamaana nyie mmekaa tu hamuwatembelei waliowaajiri pale kujua wanafanyaje kazi zao alisema jamaa.

Ali yakuti muandishi  wa filamu yenyewe
Pia tuliongea na ali yakuti ambaye ni muandishi wa filamu hiyo,kwanza alianza kwakusema yeye ameshangazw kuona watu wanaandika na kuongea mabaya wakati hawajaiona filamu yenyewe tulipotaka atuelezee kilichopo ndani yakuti alisema story ya filamu hiyo inahusu fadha ambaye hakuwa na imani thabiti na kujikuta akiyumbishwa iman yake na sister ambaye hakuwa na wito hata tone wa kuwa sister ila alilazimishwa na baba yake.

hili ni gazeti liliolandika juu ya njama
Alisema filamu hiyo ina mafunzo na kwamba katika watu waliotakiwa kuiombea itoke ni waroma kwani tumewaonyesha jinsi ambavyo wakati mwingine wanaweza kuwapokea ma sister au ma padri ambao hawana wito,yakuti alitukumbusha kuwa ni hivi juzi tu sister ambaye aliacha u sister huko sumba wanga kwa sababu hakuwa na wito kisha amefumaniwa na mume wmtu na kesi ipo mahakamani sasa yakuti anahoji sister kama huyo aliyeamua kuacha kama angekuwa na baba mwenye msimamo akamngangania una dhani angefanyaje ili kuondoka angewe kufumwa na mwanaume hata hapo hapo kanisani au angebeba mimba ili kuwaonyesha kuwa hataki tena utawa,,,,sasa nashangaa kuona wanasema tumevuka mipaka wakati haya mambo yapo wazi kabisa na yanatokea alimaza yakuti.

Tulipomuendea hewani ray hakupatikana ila tulimpata johari ambaye alisema amesikia watu wakisema ila yeye bado anajuwa movie itatoka wadau wakae tayari wala wasiyajali maneno ya watu wasiyojuwa alimaliza johari

No comments:

Post a Comment