Saturday, January 26, 2013

RAY AITUHUMU SEREKALI AWAOMBA MASHABIKI WASILALAMIKE KUHUSU FILAMU ZA MAPENZI..ASEMA NYUMA YA PAZIA KUNA MAMBO

Ray akiwa kazini
Muigizaji nyota na mwenye mafanikio ndani ya bongo amefunguka na kuitupia serekali lawama kwa kushindwa kusimama kwa ajili ya maslai ya msanii na kumuacha akionewa na kukosa uhuru wa sanaa yake ambayo ni kioo na ni darasa kwa wengine.
Gresi mapunnda sister mkuu akitowa maelezo kwa watawa

Ray ameandika katika moja ya status zake jambo lililofanya wengi kutafsiri status hiyo na sakata linaloendelea kati yake na wakristo walionyesha kutopendezwa na filamu ya ray ijulikanayo kama sister mery,ambayo imechezwa katika mazingira ya dini ya kikristo ambapo ray amecheza kama faza na uwoya na johari na wengine wamecheza kama masister.

Filamu hiyo ambayo imeshakamilikia kila kitu ilitegemew kutoka mwezi wa kumi na mbili mwaka jana ila kutoka na matatizo ya hapa na pale filamu hiyo ilizuiliwa na kufikia hatua ya sakata hilo kufika bodi ya filamu na pale basata baada ya ray kwenda kuwastakia ila chaa jabu wanaonekana kama wameshindwa kupambambana ili filamu hiyo iweze kuingia sokoni.

Mzee masinde ndiye alicheza kama baba askofu
johari akiwajibika
Kumbukumbu zinaonyesha kuwa hii ni filamu ya pili kwa ray kuingia katika mizozo baada ya ile iliyohusisha dini ya kiislamu iliyokwenda kw jina la Divoce ambayo waislamu nao walitowa malalamiko  wakidaia haikuwa sahihi kwa ray kutengeneza filamu ile japo kwa baadae walimtaka ray aipeleke kwa mashekhe wakaitazame kama haitakuwa inaupotosha uislamu na baada ya kujiridhisha kuwa hakuna jambo baya walimruhusu kuitowa kwa baraka zote.

Akizungumza na sisi mtu wa karibu na ray ametuambia kuwa ni kweli filamu hiyo ina migogoro iliyosababisha ray kukutana na katibu wa kadinal pengo na kufikia hatua ya kutokuelewana kitu kilichofanya ray aandike barua katika ngazi husika akipinga kuzuiliwa kwa filamu yake hiyo.

Katika ukurasa wake ray ameandika ujumbe huu ulionyesha dhahiri anaumia kwa kitendo kileRay Kigosi   Wadau m2ache 2endelee kucheza movie za nmapenzi coz Tanzania amna uhuru wa uigizaji so msilalamike nyuma ya pazia ni hatari sana

 • Watafiti wa maswala ya sanaa waliongea na sisi  na kusema si sawa huku wengine wakieleza kuwa kwa kawaida nchi zote jambo la kuziya filamu ni jambo la bodi na siyo mtu mmoja au kikundi flani maan ikiwa hivyo basi hata hizi story zinazochezwa kuhusu wachawi wanafunzi kutowa mimba ukimwi na watoto wa mitaani,majambazi na mambo kadha wa kadha basi ingebidi tuwapelekee waone ili waruhusu hii sio sawa.
  Ray akitowa maelekezo kwa wasanii
  Vijana wakiwajibika
  mark mwanasanaa anayeishi na kufanya sanaa yake marekan amesema  yeye anachojua kama bodi haitaki hiyo filamu huwa wanapiga gharama wanakurudishia pesa zako kisha unaambiwa uifute ile filamu sasa nitashaangaa sana kama munamuambia ray asitoe filamu ambayo katumia mamilioni ya shilingi alafu mumuambie hamuitaki yeye pesa yake anaipataje.

  Katika hili ray aliwahi kukaririwa na vyombo vya habari kwakuilalamikia serekali kwa kutokujali msanii anapopata matatizo ray ameeleza kusikitishwa kwake kwa kile alichokiita kutokujitambua kwakuwa msanii anapopatwa na tatizo kama hilo mara nyingi bodi husika ndio inapambana kwa hilo sasa leo eti mimi ndio na hangaika wakati tuna kosota tuna bodi ya filamu.

  Tulipata nafasi ya kumpigia mwakifwamba ambaye ni raisi wa shirikisho la filamu nchini tanzania na kukiri kulipata hilo mezani kwake na analishughulikia kuhakikisha msanii wake hapotezi haki zake    Tulipomuhoji johari kuhusu nguo zilizotumika katia filamu hiyo alisema kila kitu unachokiona ni cha kampuni tuligharamia kila kitu sasa nitashangaa sana kama watasema tumetumia nguo zao sisi kila kitu nichetu alisema johari kwa msisitizo

No comments:

Post a Comment