Saturday, January 26, 2013

SITER MARY YA MZULIA RAY BALAA.....SOMA KILICHOMKUTA

Mapadri wa kanisa katoliki wasema isingie sokoni Ray achanganyikiwa asema nimetumia pesa nyingi sana lakini sina la kufanya

VICENT KIGOSI,, RAY

  Kikao kizito cha saa 5 kilichofanyika Jumanne iliyopita katika Ofisi za Utamaduni jijini Dar es Salaam. Hakikuzaa matunda kwa msanii wa filamu bongo vicent kigosi alimarufu ray kutokana na kutoelewana baina yake na mapadri wa nne ambao walitumwa na kadinali pengo kuifuatilia inshu hiyo.

Kikao hicho ambacho kilihudhuriwa na mkurugenzi Mtendaji wa Utamaduni aliyetajwa kwa jina moja la Mwansoke, mapadri wanne na mtu mmoja aliyedaiwa kuwa ni mtu kutoka Ofisi za Usalama wa Taifa walijikuta wakikosa majibu ya kilichowaweka pale mara baada ya mapadri hao kupandisha mori na kutotaka muafaka.

Hivi karibuni viongozi wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam walimtaka ray  aandike barua itakayoelezea ni kwa nini mtawa Sister Marry ameonyesha matendo ambayo kiuhalisia, Wakatoliki wenyewe hawayafanyi.lakini cha kushangaza kabla Ray hajapeleka hiyo barua ndipo alipopata ujumbe uliyomtaka kufika katika ofisi hizo huku akiwa na filamu husika kwaajili ya makubaliano.
Ray aliitikia wito na alipofika wajumbe waliiweka filamu hiyo yenye masaa matatu 3 na kuanza kuingalia kwa makini hadi mwisho huku badhi za sehemu zikiwafanya wale ma padri kujikuta wanaguna.

 
Filamu ilipokwisha ndipo mwansoke aliporuhusu hoja  mapadri wakasema ‘noooo’. Filamu hiyo isiende mitaani hata kidogo kwani imejaa udhalilishaji wa Wakatoliki.
No! hii filamu kwakweli tunaomba isitoke na kama kuna uwezekano izuiwe na serekali huu ni udhalilishaji alisema padri huyo.
Ulipofika wakati yule jamaa wa uslama wa taifa nae alichangia kwa kusema kuwa kabla ya kifungia filamu yenyewe lazima muainishe kwanini mnataka ifungiwe sasa kwakuwa hapa tumekuja kujadili naomba muniambie sababu za kuizuiya filamu hii isiende sokoni.hapo ndipo hoja zikaanza. Mwansoke akasema vipande vyote vichafu vinyofolee na kubaki vile ambavyo wajumbe hawakuvigunia.
Hapo ndipo aliposimama paroko wa kanisa la Mtakatifu Maximilian Kolbe lililopo Mwenge Kijijini nakusema kwanza mambo yaliyonyesha humu si ya kweli na ukristo haufanyi hayo mambo,, pili filamu hii imeshutiwa katika kanisa langu  sasa kama atataka kuipeleka sokoni kwanza naomba afute vipande vyote vinavyoonyesha kanisa langu.maneno hayo yalimuumiza sana ray.
Ray alipohojiwa kuwa ana mawazogani juu ya kufuta vipande hivyo alisema kuwa haitawezekana kwani asilimia 85 ya filamu hiyo imeshutiwa katika kanisa hilo sasa ukishavifuta kutakuwa hakuna tena filamu kwa hiyo wakisema hivyo wanamaanisha filamu iwe na dakika tano tu 5 inawezekana kweli alihoji ray.

  Msanii huyo pamoja na kuwaeleza wajumbe kuwa katumia pesa nyingi katika kuitengeneza filamu hiyo bado haikusaidia kitu mpaka wanatawanyika majibu yalikuwa ni ray kufuta hiyo asilimia 85 ya filamu ya kwani mapadri hawakuta kuelew kitu na kusema kama ray anaona kaonewa na aendea mahakamani ila wao hawaitaki hiyo filamu walipomaliza waliinuka na kuondoka huku kikao kikikosa muafaka.

No comments:

Post a Comment