Thursday, January 24, 2013

STEVEN SANDHU KUWAANGALIA WAZEE.

Steven Sandhu
Steven Sandhu mwigizaji na mmiliki wa kampuni ya Triple S Entertainment.
MSANII Nyota katika tasnia ya filamu Swahiliwood Steven Sandhu amegeukia huduma za kijamii zaidi baada ya kufungua kampuni yake inayojulikana kwa jina la Triple S Entertainment, anasema kampuni hiyo pamoja itajihusisha na masuala ya filamu na burudani kwa ujumla lakini kazi ya kwanza ambayo kampuni hiyo inaanza nayo ni kusaidia Wazee wasiojiweza.
a ya CPU filamu kubwa 

“Kampuni yangu itakuwa kama zilivyo kampuni nyingine lakini tofauti ni kwamba sisi tunaangalia maisha ya Wazee kwa ajili ya kuwasaidia, kundi ambalo nahisi limesahaulika kabisa, kwani taasisi nyingi zinajaribu kuangalia akina mama na watoto si jambo baya lakini sisi tunageukia Wazee kuwawezesha,”anasema Steve. Triple S Entertainment yenye makao makuu jijini Dar es Salaam na tawi lake likiwa Jijini Arusha itaanza kazi zake Jijini Arusha, tayari timu yake ipo Arusha kwa ajili ya kutafiti ni Wazee gani wenye sifa za kusaidiwa na kampuni hiyo, pia Steve anasema kuwa kampuni yake inafanya kazi za kurekodi filamu na kuandaa matamasha.

No comments:

Post a Comment