Wednesday, January 23, 2013

"UNDER THE SAME SUN" WAUTAMBUA MCHANGO WA FID Q WAMTUNUKIA CHETI MAALUMUHapa Fid Q AKIPOKE CHETI HICHO TOKA KWA PETER ASH
Yule mkali wa mashairi alissiyeishiwa swaga za kuflow kutoka jiji lenye miamba Mwanza, Fareed Kubanda a.k.a Fid Q au ngosha kama anavyopenda kuitwa ametunukiwa cheti maalum cha shukurani na shirika linalosaidia watu wenye ulemavu wa ngozi(albino) linalojulikana ma Under The Same Sun kwa mchango wake mkubwa katika kusapoti kampeni ya shirika hilo.
FID Q AKIWA NA FAT JOE MKALI TOKA MAJUU
 
Ngosha ambaye aliingia vitani na watasha hao kupinga mauwaji hayo huku akisema ni bora kukosa shoo lakini nifanye kitu kwa ndugu zangu.
Fid Q amepost picha akiwa na mwanzilishi na mwenyekiti wa shirika hilo la Canada,Peter Ash, na kuisindikiza picha hiyo na maandishi yanayosomeka "Just received CERTIFICATE OF APPRECIATION from the one and only Mr. Peter Ash (CEO of Under The Same Sun).


MOJA YA POZI ZA FID
Fid Q Ametunukiwa cheti hicho kutokana na mchango aliouonyesha wakupinga mauwaji ya albino kwa vitendo,waandaaji hao wamesema wao wameridhiswa na mchango wa mwanamuziki huyo na kudai kuwa fid alijitowa sana na kuungana nao bila kujali kipato akahakikisha iwe usiku au mchana anazunguka kupinga mauwaji hayo.

HAPA AKIWA NA KIKWETE 2010 KATIKA KAMPEN
Fid ambaye ni mzaliwa wa mwanza aliwahi kukaririwa na vyombo vya habari akisea binafsi nawachukia sana hawa watu wanaofanya hivi vitendo natamani ningekuwa na maono ya kinabii ya kuwatambua ,basi wangeomba aridhi ipasuke kwa adhabu zangu,aliendelea kusema,,,,we huwezi mchinja binadamu mwenzio kama kuku yaani unamwinda kama swala huu ni ubinadamu wawapi kweli alisema Fid kwa uchungu.


HUYO NDIO FID Q HAYA KAKA


Mwaka jana Fid Q  alifanya ziara akiwa na wasanii wengine wa muziki wa kizazi kipya nakuzunguka mikoa ya kanda ya ziwa kwa ajili ya kuwahamasisha watu kupinga mauaji ya albino wakiwa na shirika hilo huku yeye akiita zizra hiyo jihadi ya nafsi kwa wenzetu.

Miezi kadhaa baada ya ziara hiyo Fid na wenzake huku wakiwa chini ya usimamizi wa shirika hilo la wa hisani walirudi tena huko katika mikowa ya kanda ya ziwa kuwarudishia wananchi waishio mikowa hiyo shukurani  sababu mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) yalipungua sana, hivyo kudhihirisha kuwa kampeni yao kwa kushirikiana na wakaazi wa kanda ya ziwa ilifanikiwa kwa kiasi kikubwa.

No comments:

Post a Comment