Wednesday, January 23, 2013

WASANII WA BONGO MOVIE WAIONGELEA STEPS

Picha ya pamoja ya wasanii walio steps
Wakati soko la filamu likizidi kuchukua nafasi na kupata mashabiki wengi ndani na nje ya nchi yetu kampuni ya steps inayoaminika kuwa ndio kampuni mkombozi kwa wasanii japo wengine wasiokuwa na lebo pale steps wamekuwa wakilipinga hilo na kusema kuwa kampuni hiyo imekuja kuuwa soko la filamu nchini.

Msanii wa filamu cluod 112
Wakizungumza na sisi kwa wakati tofauti wasanii hao waliojigawa katika makundi mawili walisema kuwa bado kiliochao kwa serekali ni kikubwa sana na hakuna wasanii waliofanikiwa duniani pasipo mkono wa serekali yao.

masanii wa filamu Riyama Ally
Akizungumza na sisi msanii riyama ally alisema yeye ni msanii na hana upande wowote ule yeye anategemea ma produser watakaomuita kucheza bila kujali wapo steps au lah!Riyama aliendelea kusema anasukuru kwa picha yake kukaa kwenye bango la steps kipindi kile japo hafungamani na upande wowote yeye yupo kote kwani bado yeye ni kioo cha jamii popote iwe saloon au nyumbani atakuwepo tu alimaliza riyama na alipotakiwa kueleza kama kampuni hiyo imesaidia alisema ndiyo maana wakati hawa jamaa (steps)hawajaja tulikuwa tunafanya movie kwa kiwango cha laki tatu hadi milion tatu sasa watu wamefika hadi milion arubaini na tano bila kutaja ninani anayelipwa pesa hiyo.

Kwa upande wa cloud 112 alisema yeye anachojua steps wamesaidia kwa kuwastua watu kuwa filamu ni pesa ila anadai bado pana hitajika mtu mwingine mbadala ili soko likuwe hatuwezi kuwa na mtu mmoja tu maana patakuwa hapana ushindani.

Msanii wa filamu rich rich na Bosi wa steps Dilesh
Rich Rich yeye alisika akisema kwa sasa hakuna kapuni inayojali na kuwalipa pesa nyingi wasanii tena kwa wakati kama steps...kaka wacha kaka kampuni ya steps ni kiboko we kapuni gani inayoweza kuwalipa wasanii mamilioni ya pesa kulingana na kazi yake,sisi tumetoka mbali sana kaka tulikuwa tunalipwa mion tatu kwa sinema alisema richi.

Dk Cheni alisema steps amekuja kuwafungua wasanii watanzania macho na hata akitokea msambazaji mwingine hawawezi kurudia makosa ya zaman bali wataendeleza yale mazuri ya steps alisisitiza cheni.

msanii wa Jacob stephan Jb
Jb alisema kila kitu ni shani toka kwa mungu ,Unajua mungu akiamua kusema na wewe basi hachagui wakati wala sehemu ya kukuambia ..mungu yeye husema kwa wakati wake .Unajua steps ni kama mungu alimleta kwetu ili kuonja matunda yetu tumeteseka sana tumelia sana na serekali yetu ila ni kama ilikuwa imefumba macho kwetu hadi steps alipoamua kujikita kwetu nakutuondolea angalau ile aibu ya msanii kutembea kwa miguu kwa kukosa nauli ya dala dala sasa kwanini mtu kama huyo usimuombee kwa mungu.

Msanii wa filamu jacklin wolper
Jackline wolper yeye alisema anamsukuru mungu na anamini mungu aliyemleta steps atawaleta na wengine ili kukuza soko letu kimataifa zaidi alisema jack.

Msanii wa filamu vicent kigosi Ray
Ray Wanaomponda steps hata siwaelewi maana kila kukicha utasikia steps mwizi anawanyonya wasanii ninachojiuliza ni kwamba steps hajatuita ila sisi tumeenda wenyewe sasa nyie mnaotuonea huruma sisi tunawaomba mutuletee mwenye huruma na sisi yaani zaidi ya steps maana kuongea wasanii wanaibiwa haisadii ikiwa huna uwezo wakutusaidia.Raya aliendelea kusema leo pesa tunayolipwa ni ndogo lakini huwezi linganisha na hawa wasambazaji wengine leo angalao msanii wa tanzania naye anamiliki hata usafiri wake mwenyewe japo watu watasema ni kawaida au wenzetu wa ulaya wanamiliki zaidi ya tulivyonavyo sisi ila tufahamu sanaa ya tanzania tunapambana nayo wasanii wenyewe tofauti na wenzetu serekali yao ndio inayopigania zoezi hilo alimaliza ray.

Msanii wa filamu Irene uwoya
Uwoya alisema tu kuwa hakuna kama steps kwa sasa lapda kwa baadae maana huko kwingine movie umetumia milion ishirini na saba mtu anakuambia anakupa miliona 6 yaani ni kichekesho niliwahi kupeleka movie yangu kwa msambazaji flan jina kapuni alipojua gharama nilizotumia akaniambia hii siiwezi mpelekee steps kwa hiyo inamaanisha wao wenyewe wanajua kuwa steps ndio mpango mzima.

Msanii wa filamu Aunt Ezekiel
Aunt Ezekiel alisema yeye amefanya kazi nyingi na steps na anayafurahiya malengo yao kwa wasanii wa tanzania kwa hiyo anaamini kila kitu kitakuwa poa alimaliza mwadada huyo ambaye kwa sasa ni mke wa mtu.

Msanii wa filamu baba haji
Baba haji yeye alisema mimi nimewahi kuwa msambazaji nalijua vizuri soko ukiona mtu anaweza kuwalipa wasanii pesa nyingi na kwa wakati kama afanyavyo steps basi ujue ana akiba yake sio kwa kutegemea filamu yako kwani mara nyingi soko la filamu ni mali kauli wanaolipa keshi ni wachache sana alisema baba haji ambaye kwa sasa yupo bagamoyo chuo cha sanaa akisomea maswala yote ya filamu na sana ya majukwaa.

kwa upande wa kampuni hiyo msemaji kambarage amesema yeye hana hoja ila wasanii watanzania waneteseka sana na kampuni yao iliona hilo na kuamua kuwasaidia kwa kufanya nao biashara sisi faida yetu ndi ndogo sana ni kama tunasaidiana.

 Tulimuuliza kuhusu kanumba akajibu kanumba ni msanii anayefanya vizuri sokoni hadi leo hivyo ndio maana huwa hata kwenye mapango yetu badu tunamuweka kwa makubaliano na familia yake

kambarage amewataka watanzania kuwaunga mkono wasanii wao kwani kununua cd orijino itafanya soko lipande kwa kasi na kufanya wasanii hao kuingiza pesa nyingi zaidi.

No comments:

Post a Comment