Wednesday, January 30, 2013

WASANII WAMIMINIKA KUMTAKA LULU KATIKA FILAMU ZAO...WENGI WAONGEA NA THE SUPER STARS TZ

Lulu


Baada ya msanii elizabeth michael (LULU) kuachiwa jana kwa dhamana amekuwa dhabu inayongaa kwa wasanii wenzake hasa ma produser wa filamu, lulu sasa anagombewa na kila produser akitaka kufanya naye kazi hii inaonyesha kuwa kama lulu atajipanga anaweza kuingiza mkwanja mrefu kwa kipindi kifupi sana kama atakuwa na msimamizi mzuri
Msanii Jackline Wolper
Akizungumza na the superstars nyumbani kwake jack Wolper  alisema amefurahi sana kuona msanii mwenzake kaachiwa huru japo kwa dhamana,Nimeaandaa kitu kwaajili ya kumpongeza lulu na ninaamini filamu nitakayomchezesha itamfanya apaate faraja na kuona tupo pamoja nae alisema jack mwanamke anayeaminika kuwa ndiyo mwanadada mwenye mkwanja mrefu kwa wanawake wa bongo movie.Jack alisema kuwa anamtarajia lulu atafanya vizuri sana katika filamu hiyo kwani tangu awali alikuwa ni mkali hivyo hapa naamini atafanya vizuri zaidi kwani alimisi camera.
Jack aliendelea kusema binafsi amempokea lulu kwa mikono miwili na amefurahiya dhamana ya lulu kwani kulea alipokuwepo sio pazuri na ukiangalia lulu bado ni mtoto japo yaliyomkuta ni makubwa na ya kusikitisha sana.
Wolper ambaye anashikilia taji la ijumaa sex girl amesema filamu hiyo anaamini itapendwa na watanzania kwa jinsi stori na matukio yalivyopangiliwa na ukizingatia ndio itakuwa filamu ya kwanza kwa msanii huyo kucheza mara baada ya kutoka jela alisema mwanadada huyo.
Msanii Rose Ndauka
Wasanii walionyesha nia ya kuchezasha lulu katika filamu zao ni pamoja na mwanadada rose ndauka ambaye aliiambia thesuperstars kuwa  kwake ni faraja kuona lulu kaachiwa na ana amini huu ndio wakati wake wakukaa na kumkumbuka mungu kwani bila ya mkono wa mungu kamwe lulu asingefunguliwa ile milango na kutoka nnje rose aliendelea kuleta stori kuwa wasanii sasa ni wakati wakuwaa nae karibu na kumfariji lulu kwa kila hali ili ajione kuwa kweli yupo huru kwa sasa japo bado kesi yake haijaisha ila naamini kama tutakuwa nae karibu basi atajihisi yupo huru zaidi
Rose alisema umri wa lulu bado ni mdogo sana na anachoamini lulu ana nafasi bado katika jamii na kinachotakiwa ni kumuweka chini na kumtengeneza alipokosea ili kuyaweka sawa maisha yake alisema msanii huyo.

Msanii Jacob Stephan (JB)
Kwa upande wa msanii jb  alisema kwake yeye kama baba wawasanii bado anamini kuwa mwanaye huyo anahitaji nafasi kwa jamii na kumuona kama mtoto wao kwani hata kiumri ukiangalia bado ni mdogo hivyo anadhani huu ni wakati wa lulu kuwa mcha mungu na kujikita zaidi katika kazi kwani bado wanamuhitaji kwani nafasi yake kama lulu ipo pale pale kwa hiyo huu ndio muda muafaka kwake alisema jb ambaye anafuhi sana ukimuita Erik ford au bonge la bwana.

Msanii Single Mtambalike (Rich Rich)
Msanii single mtambalike Rich alisema kuwa anamshauri lulu kuwa mtulivu sasa na kujipanga kwani kila mtu atamuhitaji kwa sasa hivyo angalie maisha zaidi na si umaarufu kauli ya msanii huyo imetfriwa na watafiti wa maswala ya sanaa kuwa lulu akiwa makini anaweza kuingiza pesa nyingi sana kwa sasa kuliko msanii yoyote tanzani kwa upande wa filamu.

Msanii Johari
Johari alipohojiwa alisema anamuombea tu kwa mungu johari ambaye ukimkumbusha habari za kanumba hujikuta akilia kila wakati amejikuta akiwa hana raha toka kifo cha msanii mwenzake ambaye walikuwa kama ndugu na johari aliwahi kukaririwa akisema kanumba ndio msaada mkubwa kwake kwani baada ya cheni kumsaidia kupata nafasi  pale kaole na kumtetea aweze kucheza kanumba ndio aliyemuita kwa mtitu ambapo walicheza johari iliyompa jina ambalo jina hilo alilitowa msanii chopa wa mchopanga.
Msanii hissan Muya (Tino)

 Kwa upande wa tino amesema anaamini lulu ana nafasi nyingine kwani mungu kampendelea na kumpa muda wakujirudi,tino ambeendelea kusema huu ni wakati wa wasanii wote kumrudia mungu kwani leo yamemkuta lulu kesho yatakuwa kwetu,akiongea kwa njia ya simu tino ambaye yupo kambini akimalizia filamu yake amesema yeye binafsi anamsubiri akitulia atamuita kwaajili ya filamu yake ila amekanusha kuwa anamchukua kwaajili ya kuuza kwani amesema anajiamini sana na hata wadau wake wanamuamini hivyo kumchezesha  lulu ni njia moja wapo ya kumrudisha sokoni na kumuongezea kipatoalisema msanii huyo ambaye sasa amegeukia kwenye filamu za action.

 Msanii Zamda Salum
 Akizungumza na sisi toka finland msanii wa filamu bongo zamda salum amesema amefurahi sana na na anaamini wasanii wenzake watamuunga mkono lulu ambaye kwa sasa yupo katika wakati mgumu zamda amesema anamuombea msanii huyo kwa mungu ili ampe uvumilivu katika kipindi hichi na kusema anataman angekuwa hajazuiliwa kusafiri angempa ofa akapumzike kwa muda,,natamani kama masharti ya aliyopewa lulu yangemruhusu kutoka ningempa ofa aje apumzishe akili kwanza alisema zamda.

Msanii juma Chikoka
 Kwa upande wa chopa alisema hana la kusema ila mungu amsaidie na jamii ikubali kuwa lulu anarudi tena kwao na impokee,alisema bwana juma chikoka.

No comments:

Post a Comment