Monday, February 11, 2013

ALI KIBA ASEMA ANAMUHESHIMU SANA ABDU KIBA KWAKUWA UWEZO WAKE ANAUJUA

ALI KIBA NA ABDU KIBA
Msanii wa muziki nchini tanzania ali kiba amefunguka na kusema kuwa yeye alijua mapema kuwa mdogo wake anayejulikana kwa jina la Abdu kiba angekuwa msanii na siku moja watu wangemjua

Akipiga stori na blog hiii msanii huyoa mbaye anaaminika pia ni kati ya wasanii wenye mkwanja mnene tanzania Kiba amesema toka wakiwa wadogo Abdu alionyesha njia ya kuwa mwanamuziki na mimi nilionyesha dhamira yakuwa mchezaji mpira wa miguu ila cha kushangaza nilibadilika na kuwa muimbaji huku abdu akiwa mcheza mpira

Kiba anasema hashangai kuona Abdu anaimba kwani wengi walijua kuwa atakuwa muimbaji toka mwanzoni kiba amefunguka na kusema anamshukuru mungu kwakumfikisha hapo alipo na pia anamshukuru kwakumpa kipaji yeye na mdogo wake.

Kiba na Abdu ni ndugu wa damu na ni marafiki wakubwa sana ni watu wanaofanya mambo kwa ushirikiano sana na hata wakati mwingine unaweza usijue kama ni ndugu kwani mambo mengi hufanya kwa ushirikiano mkubwa sana

ABDU KIBA NA KAKA YAKE ALI KIBA
Kwa upande wa Abdu kiba ambaye alianza na ngoma ya Huyo sio Demu aliyomshiriksha Ney wa mitego na Neiba, kisha ikafuata Kizungu zungu aliyofanya mwenyewe na kuwashika watu vizuri sana, Hakuishia hapo aliachia ngoma kama Hatuna habari nao na sasa anatamba na ngoma yake ya  Kidela aliyomshirikisha Ali Kiba ambaye ni kaka yake,Kidela inafanya vizuri sana na ni kati ya nyimbo zinazo ombwa sana redioni kwa sasa.

Abdu anasema  hadhani kama ana rafiki mwingine wa karibu sana kama alivyo kaka yake huyo na katika marafiki wake wakubwa ambao hawezi kuwaficha kitu ni kaka yake huyo Abdu anaendelea kusema kuwa akiwa na kaka yake anajisikia vizuri sana tofauti akiwa na marafiki wengine ,Abdu aliendelea kusema kuwa kaka yake huyo ni kati ya washauri wake wake wakubwa sana na hata katika nyimbo zake ni lazima kaka yake ashiriki kwa namna moja au nyingine kwa hiyo anamkubali sana na pia kaka yake anamkubali pia

Kwa sasa ali kiba anajianda kwa safari ya kuzunguka nchi za ulaya kwa ajili ya shoo zake na ameiambia thesuperstarstz kuwa katika ziara hiyo ataongozana na mdogo wake katika nchi mbili kisha yeye atasonga mbele,kiba anasema anajitaidi kuwashawishi waandaaji hao ili wamuongezee nchi za kupiga shoo mdogo wake huyo ili ajitanue na kujitangaza zaidi.

No comments:

Post a Comment