Sunday, February 24, 2013


USHAURI WA BURE KWA WASICHANA WANAOVAMILA FANI YA SANAA KWA KUUZA MIILI YAO


KUTOKANA na baadhi ya wasichana wengi kukata tamaa na kutofikisha malengo yao katika sanaa hususani upande wa muziki sababu inayopelekea kushindwa kufikisha malengo yao ya muziki na kuishia njiani tofauti na ilivyotegemewa

Hali hiyo imechangiwa na baadhi ya wasichana hao ambao wanajiingiza kwenye maswala ya muziki bila ya kujua thamani yake na kuamini kutumia mwili zaidi kuliko kipaji alichonacho na matokeo yake wanakosa nafasi ya kufanya vizuri kwenye muziki

Hayo yalielezwa na msanii wa miondoko 'Zook'anayejulikana kwa jina la Vumilia, jijini Dar es Salaam wakati anaelezea sababu zinazopelekea wasichana kuwa wachache kwenye muziki tofauti na wanaume na waliokuwepo pia baadhi yao kutofanya vizuri

Alisema kuwa sababu ya kutofanya vizuri kwa baadhi ya wasichana wengi ambao wapo kwenye 'gemu' hilo ni kutokana na kutojiamini na baadhi yao kufanya vitu vya aibu ili waweze kupata jina na muziki wao kupigwa

Hali inayopelekea kuwa kwa sababu hawana vipaji wanajikuta wanapotea kwa muda mfupi kwenye gemu hilo huku wakiwa wamejishushia heshima yao kwa kutumia miili yao ili waweze kufanikiwa kwenye muziki

Vumilia alitoa wito kwa baadhi ya wasichana ambao wapo kwenye muziki tayari na wengine wanaotaka kuingia katika sanaa hiyo ni kuwa wavumilivu kuamini unachokifanya bila ya kusahau kufanya mazoezi na kujifunza zaidi ili uweze kufanikisha malengo yako kwa njia iliyo sahihi

Msanii huyo ambaye ametamba na nyimbo tatizo ni umasikini ameachia ngoma nyingine inayojulikana kwa jina la 'Dushedushe'iliyotengenezwa na Ema Theboy

No comments:

Post a Comment