Sunday, February 03, 2013

DIAMOND ASEMA HAMJUI MGANGA ALIYEJITOKEZA NA KUSEMA ATAMSHUSHA..AWAOMBA MASHABIKI WAKE WAPUUZIE

MSANII DIAMOND
Msanii wa mziki na mwenye mashabiki wengi kwa sasa afrika mashariki Diamond amefumgaka na kuiongelea ishu inayomkabili baada ya ustadh Yahaya Michael kujitokeza na kusema kuwa yeye ndiye mganga wake na kwakuwa msanii huyo ameanza dharau basi wakati wa yeye kumshusha umefika.

Akizungumza na thesuperstarstz kwa njia ya simu kutoka kigoma ambako yupo huko kwa shoo maalumu ya ccm  msanii huyo amesema kuwa yeye kama nasibu hamjui mtu huyo na wala hana story hizo ila anaamini kinachompandisha ni mungu na mashabiki wake ambao hawalali kila wakisikia ndugu yao napiga hatua Unajua kaka kusema kweli nimesoma jana kwenye blog yako hii nikashangazwa na habari kuwa kuna mganga anasema kanipandisha na ndio maaana uliponipigia jana nikakujibu kimkato ila naomba waambie mashabiki wangu kuwa haya ni majaribu kwangu na simjui mtu huyo  na kupitia  kwa mungu nitashinda tu.

Ustadhi yahaya alijitokeza jana na kusema kuwa yeye ndio mtu aliyemtowa Dimond na kwa sababu msanii huyo ameanza dharau basi  yeye anajua mbinu ya kumshusha Ili mashabiki wake wasimpende tena.

Dimamond amesema kuwa kwasasa yupo kazini huko kigoma na kusema Kaka namaliza tu shoo nikimaliza nitakutafuta tuliongelee kaka alafu nina mambo mengi sana ambayo nataka mashabiki wangu wajue kuhusu mimi kwani nahisi kuna watu wanawapotosha watu kuhusu habari zangu ila nachomshukuru mungu ni kwamba mashabiki wangu wameamua kuwa pamoja na mimi ndio maana hata wakisema wamekuwa wanapuuzia.

Diamond amemfananisha mganga huyo na mtu asiyekuwa na akili kwani hata kama unataka umaarufu hautafutwi hivyo mimi ni mtu wa watu na wala sintabishana na yeye kwani mashabiki wangu wapo makini na nina amini watazungumza nae na atapambana na mashabiki zangu alisema msanii huyo.

Mara baada ya kumalizana na Diamond tulimtafuta shekhe yahaya Michael ila hakupokea simu tulipompata mtu wa karibu na yeye ali jibu kifupi na kusema ustadhi anafanya kazi piga baadae.

Watafiti wa mambo ya kisanii tulioongea nao walisema kuwa kwa sasa msanii Diamond yupo juu na swala la kushuka kwake au kupanda kwake ni mashabiki wake na si mtu binafsi.

Wachangiaji wa mitandao ya kijamii wengi wameonyesha kutofurahishwa na jambo hilo na kujikuta wakiandika maneno mabaya kwa mganga huyo huku wengi wakimuambia kama ni mganga kweli basi ajigange yeye ili aimbe na angae kama Diamond alivyongaaa au awasaidie ndugu zake nao wangae .

No comments:

Post a Comment