Wednesday, February 20, 2013

DIAMOND ATUHUMIWA KUMTAPELI MSANII WA RWANDA MILIONI 9

Msanii Diamond


Hivi karibuni msanii wa nchini Rwanda aitwaye Mico the Best amejikuta akiingia hasara kubwa baada ya kumlipa Diamond aliyemshirikisha kwenye wimbo wake uitwao SINAKWIBAGIWE kwaajili ya show nchini Rwanda lakini hitmaker huyo wa ‘Nataka Kulewa’ alishindwa kwenda. Show hiyo ilikuwa ifanyike kwenye mji uitwayo Remela, nje kidogo ya Kigali.

Baada ya hapo Mico amekuwa akiongea na vyombo mbalimbali vya nchini Rwanda na Tanzania akitaka apewe haki yake.
Anasema alimlipa Diamond dola 6,000 ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 9 pamoja na nauli ya ndege ya watu wanne.
Mico NA DIAMOND
“Diamond amenidharau mimi na amewadharau wanyarwanda wote waliokuja kumuona,” Mico aliiambia website ya Rwanda inyarwanda.com.
http://icyerekezo.blog.com/files/2013/01/umutaka.jpg
MATANGAZO YALIYOBANDIKWA SEHEMU MBALIMBALI NCHINI RWANDA KAMA PROMO

Amesema anataka kuzungumza na Diamond ili amrudishie fedha yake baada ya kumsababishia hasara kubwa na ameomba msaada kwenye balozi za Rwanda na Tanzania.

Mico anasema hakutegemea kabisa kama diamond angefanya vile ni mtu aliyekuwa ana muamini sana na ni kati ya wasanii afrika mashariki wanaokubalika sana nchini rwanda alisema mico.
Waandishi wa the super stars tz ambao wametanda karibu kila kona ya dunia wamezungumza na wanyarwanda kule kigali na kueleza kusikitishwa kwao na kilichotokea lakini pia watanzania waishio nchini rwanda wamesema wamesikitishwa na tabia mbaya aliyoionyesha msanii huyo kwani inapelekea tanzania kutoaminika hasa katika maswala ya wasanii na ndio maana tumejikuta hatu songi mbele.

The super stars tz bado inamsaka diamond ili ajibu tuhuma hizo ila amekuwa hapokei simu na tulipofika nyumbani kwake mlinzi wake alitujibu kuwa diamond katoka asubuhi sana huku dada yake diamond akitueleza kuwa kaka yake hayupo kasafiri toka juzi.   

No comments:

Post a Comment