Friday, February 08, 2013

FLAVIANA MATATA KALAMBA DILI JINGINE? SOMA HAPA UJUE

 

.
Taarifa ikufikie kwamba mwanamitindo wa kimataifa kutoka Tanzania Flaviana Matata ameshiriki katika kampeni za matangazo makubwa ya makampuni ya nguo ya DIESEL na EDUN ambapo kampeni inaitwa DIESEL + EDUN ilianzishwa January 2012 na muanzilishi wa kampuni ya DIESEL – Renzo Rosso – na waanzalishi wa kampuni ya EDUN – Ali Hewson na Bono.

Walisafiri nchi za Uganda na Mali na kukutana na wakulima wa pamba barani Africa, waliingia makubaliano ya kutengeneza nguo maalum zitakazotokana na pamba ya wakulima hawa wa Afrika na hivyo kuwanufaisha moja kwa moja hivyo hizi nguo zinatangazwa kama kampeni ili kunufaisha bara la Afrika.

Nguo hizo zitaanza kupatikana mwanzoni mwa march katika maduka mbalimbali nchini Marekani na sehemu nyingine duniani na hata kupitia mitandao pia zitauzwa huku Flaviana Matata ambaye aliwahi kuwa Miss Universe Tanzania anabaki kuwa mwanamitindo pekee alieshiriki kwenye hiyo kampeni akitokea Africa.

.
Kama umependa hii stori unaweza ukalike au ukatweet ili na rafiki zako waone mtu wangu

No comments:

Post a Comment