Monday, February 18, 2013

HUYU NDIO MWANAUME ANAESEMA ALIMUOA GOLDIE WA NIGERIA, HIZI NDIO PICHA ZA HARUSI ZA USHAHIDI ALIZOTOA.


.
Baada ya kifo cha Goldie Harvey msanii ambae pia alikua mwakilishi wa Nigeria Big Brother Africa 2012, mwanaume aitwae Andrew Harvey amejitokeza na kusema Goldie alikua mke wake baada ya kufunga ndoa ya siri mwaka 2005 na walikua wanatarajia kupata mtoto wao wa kwanza 2013.
Pamoja na kwamba Goldie inajulikana alikua mpenzi wa CMB Prezzo wa Kenya baada ya kutoka Big Brother na hata Prezzo kuthibitisha mpango wa kumuoa, mume huyo amesema hakua na wasiwasi wowote kuhusu ishu zozote zilizoendelea kati ya Prezzo na Goldie manake alikua anafahamu kwamba Prezzo alikua sehemu ya mchezo, ni kama movie… na kusingetokea chochote kwa sababu Prezzo alikua anapenda tu kusema chochote ili apate attention, hata Goldie alimwambia walikua wanafanya kazi tu.
Andrew ambae ni raia wa England alikua kwenye mipango ya kuchukua uraia wa Nigeria kabla ya kuhamishiwa Malaysia ambako ndipo anapofanya kazi na kuishi kwa sasa lakini Goldie tayari alikua ana uraia wa U.K hata kabla hawajakutana na Andrew manake aliwahi kuishi na kusoma U.K
Andrew ambae yuko Malaysia kwa sasa amesema wiki hii ndio atawasili Nigeria kwa ajili ya mazishi.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
Goldie na Prezzo

No comments:

Post a Comment