Wednesday, February 13, 2013

JB AFARIKI DUNIA CHUMBANI KWAKE

R.I.P MR JUSTUS BAGUMA (JB)...

Msanii wa filamu mwenye mashabiki lukuki ndani na nnje ya dar Jb ama jacob stephen amesema ameshtushwa sana na sms pamoja na simu alizopokea ray  zikijieleza au kuuliza kama yeye ( jb) yupo hai
Jb amesema kuwa yeye yupo hai  hajafa na amesikitishwa sana kifo cha kaka yake huyo.
Mashabiki na wadau wa filamu jana walizua utata na huzuni ya ghafla mara baada ya kuanza kutumiana sms zinazosema jb kafariki huku wengine wakiwasiliana na msanii vicent kigosi ray kutaka kujua ukweli
MSANII JACOB STEPHAN (JB)ALIYEDHANIWA KAFARIKI
Akiongea na sisi kwa njia ya simu Jb amesema kuwa,,,Naomba mashabiki wangu wasipatwe na hofu kwani mimi  nipo hai na wala siumwi, jb aliendelea kutowa ufafanuzi kwamba  aliyefariki ni yule big bosi mwenye kumiliki hotel kadhaa kama,,,,JB BELMONTE  YA DAR NA YA MWANZA- AMBASSADOR CLUB,NA SAVANNAH LOUNGE,,,Kusema kweli nimepokea simu na sms nyingi sana lakini kifupi naomba kaka uwajulishe watu juu ya hili na amini blog yako inasomwa sana na mashabiki wangu sasa wape taarifa kuwa nipo hai na hakika nimeumia sana kwa kuondokewa na ndugu yangu wajina wangu kaka yangu rafiki yangu marehemu justus baguma alimaarufu kama Jb Belimonte,huyo ndio jb aliyefariki na sio mimi  alisema JB.
Taarifa za ndani zinadai Jb Belmonte  alikumbwa na umauti wakati akiwa chumbani kwake kalala huku chanzo cha kifo hicho kikiwa hakijajulikana hadi sasa

Msanii vicent  kigosi (ray) amesema yeye alipigiwa simu nyingi kuliko mtu yeyote jana na kupewa pole za kifo cha jb msanii wakati yupo nae pale ,,,Nilishangaa sana kaka yaani naona sms na simu zinaingia za kunipa pole huku watu wakitaka kujua jb amefariki kwa ajali au kaumwa kusema kweli nilikuwa na kazi ya ziada kuwaelewesha watu na wengine kuwapa waongee na jb mwenye ili kuondoa utata.
Baada ya kuona taarifa zinazidi kuzagaa ndipo Jb  ilipoamua kuwaelewesha watu kwakuandika katika ukurasa wake  kuwa....Mashabiki wangu wote msiwe na hofu juu yangu mimi nipo salama na mungu ananipenda sana,Napenda kutoa utata huu kuwa  aliyefariki sio jb mimi mcheza filamu bali ni ndugu yetu justus Baguma jb ,,Tajiri aliyekuwa ana miliki hotel kubwa ndani ya bongo
Msanii huyo wa filamu ameonyesha kusikitishwa na kifo cha wajina wake na kuwaomba mashabiki wake wasi amini sms zinazoendelea kuzagaa hovyo zikielezea kuwa jb yeye kafariki na wakati yeye yupo hai.

1 comment:

  1. Tunashukuru sana kama niuongo,poleni pia.

    ReplyDelete