Sunday, February 03, 2013

KIPAZA SAUTI CHA MZINGUA DIAMOND JUKWAANI KIGOMA

MSANII DIAMOND
Ubovu wa vyombo huko kigoma umemfanya msanii Diamondi ambaye yupo huko kwa sherehe za ccm umemfanya msanii huyo aktishe shoo na kupumzika hadi vitakaporekebishwa

Awali katibu mwenezi wa chama cha ccm bwana nape nauye alimkaribisha na kumruhusu msanii diamond alishambulie jukwaa kwa ajili ya kuwapa burudani wa kazi wa kigoma jambo ambalo lilifanya watu wapige kelele za shangwe huku wakikimbilia mbele ya jukwaa kumuangalia star huyo mwenye mashabiki kibao,walinzi wa ccm waliokuwa wakiwazuiya walijikuta wakipata kazi nguma kwani wananch walizidi kumiminika na kumfanya dimond ambaye alishuka chini kuimba nao kupandanda tena jukwaani kwa haraka.

Mara baada ya msanii huyo kuitwa na kupanda jukwaani vyombo vya muziki vilianza kusumbua na kukata kabisa jambo lilimfanya Nape kuwaambia watengeneze haraka ili msanii huyo aimbe mafundi walipambana na kufanikiwa kwa asilimia ndogo sana kwani japo msanii huyo alijitaidi kuimba ila mwisho alishindwa kwani sauti ilikata kabisa akizungumza na sisi mwenyekiti wa maandalizi ya sherehe hiyo alisema kuwa vyombo hivyo vimepata hitilafu muda mfupi baada ya raisi kuingia uwanjani jambo ambalo wasingeweza kuvitowa kwani maiki ya mc na ile aliyokuwa anaongelea raisi zenyewe hazina matatizo ila zile maik za wajumbe na zile za wageni waalikwa zilikata ikabidi kuzibadili kwa haraka na hatukujua kama na zile zimekata alisema kiongozi huyo wa ccm mkowa wa kigoma.


Raisi wa jamuhuri ya kigoma mh.jakaya mrisho kikwete alipopewa nafasi ya kupanda kwa ajili ya kutowa hotuba yake alianza kwakusema kuwa baada ya hotuba na yeye ataungana na wanakigoma kwakucheza na msanii diamond huku akitania na kusema bado hajazeeka anauwezo mkubwa wa kusakata rhumba.

Baadhi ya wananchi wa kigoma wanasema kuwa wanamkubali sana jamaa na hali iliyotekea imewakera sana na kuwataka waandaji hao mara nyingine wanapoandaa wajipange na sio kufanya kama yaliotokea leo
We msanii mkubwa kama diamond na chaguo letu unampandisha wakati hamja seti mambo yenu ningekuwa mm nisingepanda tena maana watu wenyewe hawajajipanga.

Tulimfanya mawasiliano na Diamond mara baada ya kushuka jukwani na kumuliza imekuwa akasema Maiki ya mwanzo aliyoambiwa ataimba nayo baada ya test ilihamishwa baada ya zile kule kuharibika ila naona wamejisahau ila,kwa upande wa nape anasema mara baada ya raisi kumaliza hotuba yake wakazi wa kigoma watapata shoo ya maana sana toka kwa msanii huyo ambaye nae pia anatoka kigoma.
No comments:

Post a Comment