Thursday, February 14, 2013

  MAMA LULU NA MAMA KANUMBA WAPATANISHWA...LULU AMUOMBA KANUMBA ARUDI ILI ASEME KILICHOTOKEA KUMUOKOA YEYE..KILIO CHAKE CHA MLIZA MAMA KANUMBA.


Hatimaye mama mzazi wa marehemu Steven Kanumba amepatanishwa na mama mzazi wa Lulu baada ya mlolongo mrefu na mgumu wa jitihada za kuwapatanisha kina mama hao wawili.

Chanzo chetu cha kuaminika  kimeripoti kwamba mama mzazi wa marehemu Steven Kanumba alikua mzito kupatanishwa kwa sababu ya kukasirishwa na kitendo cha mama mzazi wa Lulu ambae hakuwahi kufika msibani wala kutuma salamu za pole kwa mama Kanumba.

Baada ya Lulu kutoka kwa dhamana, mama mzazi wa marehemu Kanumba alisema yuko tayari kuonana na Lulu kwa sababu ni mtoto na hana tatizo nae lakini akasisitiza kama Lulu atakwenda kuonana nae ni sawa ila asiende na mama yake.

Wazazi hao wamepatanishwa jumapili february 10 2013 ambapo Lulu alikuepo kama muhusika mkuu wakati huo wa upatanisho, kwa siku zote mwigizaji huyu alikua akiomba kupatanishwa na mama wa Marehemu, pia alikua akisisitiza kuomba mama yake apatane na mama Kanumba,


Sababu za Mama Lulu kushindwa kwenda msibani alisema kwanza ni uoga kutokana pia na jinsi vyombo vya habari vilivyopamba, na nyingine ni machungu aliyokua nayo dhidi ya waigizaji hao wote wawili ambao alikua hajui kama walikua wapenzi, alikua anajua Marehemu anamfundisha Lulu usanii tu.

Mapatano yalisimamiwa na wazee wawili pamoja na watu wengine wa karibu wa familia na ilichukua dakika 240 kazi kumalizika kutokana na Mama mzazi wa Kanumba kuwa mgumu kiasi chake.

Baada ya kupatanishwa imeelezwa ndio mama mzazi wa Marehemu Kanumba, mama mzazi wa Lulu na watu wengine kadhaa wa karibu wa hizo familia, walikwenda kwenye kaburi la marehemu Steven Kanumba Kinondoni Dar es salaam Kwaajili ya kwenda kumuonyesha lulu alipozikwa marehemu steven kanumba The great.


Mara walipowasili makaburini lulu alijikuta akiangua kilio kilichosababisha majonzi makubwa na kufanya wote waliohudhuria kuanza tena kulia upya,lulu alilala juu ya kaburi la kanumba huku akimuomba amke huku watu wakimuinua eneo lile,Amka kanumba,Amka nikuone tena amka jamani mimi lulu kanumba kwanini lakini kanumba mbona umeniachia mtihani jaman nisaidie kanumba nisaidie kuweka ukweli watu wajue,,Waonyeshe watu waelewe ukweli nateseka mimi jamani kanumba oooohhh,,Hayo ni maneno ya uchungu na ya kilio aliyoyatowa lulu huku akilia kwa kulala juu ya kaburi la kanumba the great.

1 comment:

  1. maskini LULU pole i can feel your pain jikaze tu hamna jinsi mamangu

    ReplyDelete