Monday, February 11, 2013

MAMA LULU AMFARIJI MAMA KAJALA,,,,NAKUMTAKA KUWA MVUMILIVU...


Siku chache mara baada ya msanii wa filamu nchini kutoka mahabusu kwa dhamana, Mama mzazi wa msanii huyo wa filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’, Lucresia Karugila, hivi karibuni alinaswa akimpa mbinu mama wa msanii Kajala Masanja zitakazomsaidia kumuokoa mwanaye katika kesi inayomkabili ya kutakatisha fedha haramu.

Mama huyo alinaswa na mwandishi wetu kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo Kajala na mumewe, Faraja Chambo walifikishwa kwa ajili ya kujitetea kwenye kesi inayowakabili ya kutakatisha fedha haramu.

Mama Lulu ndiye aliyeanza kufika mahakamani hapo na baada ya muda, Mama Kajala alitokea na kisha kujisogeza  pembeni na kuanza kuteta  huku mama lulu akimpa mama kajala mbinu za kuweza kumsaidia katika kesi hiyo.

Mwandishi wetu alipowaona alijisogeza taratibu  hadi pembeni yao bila wao  kujua kama ni muandishi na kuchukuwa habari zote na ndipo alipogunduwa kuwa mama lulu alikuwa akimpa mwenzake mbinu za kumwezesha kumuokoa mwanaye kajala katika  kesi hiyo.

Naona mama Lulu anampa mwenzake mbinu za kumuokoa Kajala ila amefanya la maana sana kuja kumpa kampani na kwa uzoefu wake wa mahakamani anaweza kumsaidia,” alidai mama mmoja aliyekuwa karibu yao.


Wazazi hao walisitisha mazungumzo baada ya Kajala na mumewe kutolewa chumba cha mahabusu na kupandishwa kizimbani ambapo Wakili wa Serikali, Renald Swai aliiahirisha kesi hiyo hadi Februari 12 baada ya kupokea udhuru kutoka kwa hakimu aliyetakiwa kusikiliza kesi hiyo, Sundi Fimbo.

Baada ya kuahirishwa kwa kesi hiyo, mama Lulu aliendelea kuwa karibu na mama Kajala ila kilichowatawanyisha kilikuwa ni mwanga wa kamera .

No comments:

Post a Comment