Tuesday, February 05, 2013

MAMA STEVEN KANUMBA AJA NA FILAMU YA "WITHOUT DADDY."


MAMA Mzazi wa msanii nyota Tanzania marehemu Steven Kanumba ‘Kanumba’ Frola Mtegoa ameigiza filamu katika muendelezo wa kipaji cha mwanaye baada ya kuigiza katika filamu ya Without Daddy akishirikiana na watoto waliokuwa wakiigiza na marehemu Kanumba kama Patrick na Jamila, katika filamu hiyo mama Kanumba kaigiza katika kiwango cha juu.
.

Abdul Ahmed Jamila
Ben Blanco akiwa na wasanii wakali Jamila na mwenzake.
Akiongea na tstz mkurugenzi wa kampuni ya Big Daddy Production Irene Kaungwa amesema kuwa filamu ya Without Daddy ni kazi mwendelezo wa kazi ya marehemu Kanumba iliyotoka siku za nyuma ya Big Daddy na ni kazi ambayo imetentengezwa kwa ubora wa kimataifa ikiwa sambamba na kumtambulisha mama Kanumba katika tasnia ya filamu Swahiliwood.

“Kampuni ya Big Daddy Production imekusudia kuleta mapinduzi makubwa katika tasnia ya filamu Tanzania, na katika kumuenzi marehemu tumemchukua mama Kanumba kushiriki katika filamu hiyo na mama ameonyesha uwezo mkubwa katika uigizaji na filamu yake ya kwanza
ndio hii,”
anasema mkurugenzi.

.
Jamila
Mmoja kati ya wasanii walioshiriki katika Filamu ya Without Daddy.
Frola Mtegeo
Mama Kanumba mwigizaji.
 Filamu ya Without Daddy imeshirikisha wasanii nyota wengi kama vile Abdalah Mkumbilah ‘Muhogo mchungu’, Fatuma Makongoro ‘Bi. Mwenda’ Cathy Rupia, Mayasa Mrisho, ‘Maya’, Othuman Njaidi ‘Patrick’ Wastara Juma ‘Stara’ Abdul Ahmed ‘Ben Blanco’ na wasanii mahiri wengineo.

1 comment: