Saturday, February 02, 2013

MENEJA WA DAR STAMINA ASEMA MENGI KUHUSU KUNDI LAKE LA DAR STAMINA

SHABAHA MENEJA WA DAR STAMINA
Aliyekuwa meneja wa msanii sheta kabla ya kujitowa katika kundi la Dar Stahmina  anayejulikana kwa jina la Shabaha amefunguka na kuzungumza na thesuperstarstz kuhusu ukweli wa nyimbo zilizomtowa sheta.

Akipiga stori na blog hii maeneo ya facebook take away kwa big dady shabaha amesema kuwa anashangazwa na kauli za msanii huyo ambaye kwa kiasi kikubwa amesema kuwa yeye ndiye aliyeandika nyimbo zote zilizomtowa sheta kasoro hii ya bonge la bwana ambayo inaonekana wazi haijafanya vizuri.

NUH MSANII WA DAR STAMINA AMBAYE YUPO CHINI YA MENEJA SHABAHA
Shabaha amesema kuwa dar stahmina ni kundi ambalo halimtegemei mtu mmoja N shabaha amesema  yeye ni kama wenga  kwani akitoka mtu anaingia mtu na yeye hategemei mtu ila yeye ndio anayetegemewa huku akiuliza kuwa uliona wapi wenga anategemea mchezaji?Sheba anasema licha ya msanii huyo kufukuzwa kundi lake  lina vichwa vya maana na kuzidi kusema sheta anapaswa kuishukuru Dar stahmina kwani bila kundi hilo asingekuwa sheta wa leo kwani nyimbo zote za sheta kuanzia,Mi na play  nyimbo ambayo aliirekebisha yeye na kisha kumtafuta Mwana F.A ambaye aligoma kuingiza sauti yake hadi nyimbo irekebishwe jambo alilolifanya shabaha kisha kurudi tena kwa Mwana F.A Na kukubali kupiga korasi

Shabaha aliendelea kuzitaja nyimbo alizoziandika kuwa ni Nimechokwa aliyofanya na Bele 9 na kumtambulisha vyema Sheta,nyingine ni pamoja na Mdananda,pamoja na Ni Danganye danganye aliyofanya na Diamond,Shabaha amesema kuwa wimbo wa ni danganye Aidia na korasi ya wimbo huo alitowa kisha  kwenye vesi alishiriki  mabest.

NUH AKIFANYA SHOO YA MAANA MAISHA CLUB

Kwa sasa Shabaha anasema ili kuonyesha umakini wake na wa kundi lake la Dar stamina Anamtowa msanii mwingine anayejulikana kwa jina la Nuh ambaye ameshafanya vizuri katika wimbo kama Bwege mtozeni,mniache ambayo amefanya na Ali kiba,na sasa anatamba na nyimbo inayoitwa Feeling love ambayo kakamua mwenyewe na ni kati ya nyimbo ambazo zinapigwa sana katika redio ,Shabaha anasema wapo kwenye hatuwa ya mwisho  katika kumalizia utengenezaji  wa  video ya wimbo huo wa feeling love.

Naye msanii huyo Nuh alisema kuwa kwa upande wake anamshukuru sana meneja wake na kusema kuwa kwasasa anajipanga baada ya kumaliza video yake atazama jikoni na kushusha kitu kingine ambacho aligoma kukitaja jina.


Shabaha anasema yupo kwa ajili ya maslai ya Dar Stamina na ndio maana alijitowa kuhakikisha Sheta anatoka kisanii ...Unajua mimi nilimuandikia sheta zile nymbo ili kumtowa kisanii  lakini jamaa akavimba kichwa na kijiona yeye ndio yeye nikamshindwa nikamuambia aondoke ili nimpe nafasi akafanye mambo yake na baada ya kuondoka nadhani watanzania wamesikia nyimbo yake mpya ya bonge la bwana,hapo nadhani watanzania ndio wanapima alipokuwa na sisi na alipo hivi sasa.

Shabaha anasema kwa upande wake anamtaki kila la kheri msanii huyo na kumshauri kuheshimu asili.No comments:

Post a Comment