Tuesday, February 05, 2013

MHESHIMIWA SUGU AMSHUKIA ROMA KWA KUMTAJA KWENYE 2030:

Mwana muziki ambaye  kwa sasa ni mheshimiwa kwa tiketi ya ubunge alioupata mbeya bwana joseph mbilinyi alimaarufu kama Mr 11 au Sugu ameonyesha wazi kukerwa na msanii mwenzie roma kwa kile alichodai roma ana kurupuka na hajui anachokifanya.
 
Akizungumza nda ya EATV Katika kipindi cha friday Night Live Sugu amesema kuwa msanii huyo anapaswa kuijua misingi ya hip hop na pia Sugu amemuonya na kumtaka  roma awe muangalifu na anachokiandika na kukitowa kwa jamii na sio kukurupuka kama mtu aliyestuliwa toka usingizini.
 
Sugu amesema yeye ni mfuasi wa hip hop hivyo ukitaka kuwa mwana hip hop lazima uzame ndani sana ili ukiandika kitu uwe na uhakika nacho na si kufanya kama Roma anavyofanya.Namtahadharisha bwana mdogo awe muangalifu na anachokiandika na si kukurupuka hip hop ina misingi yake na ni lazima uzame ndani sana maana hip hop ni maisha na ukweli mtupu, pia aelewe hip hop ni sauti ya kumkombowa mnyonge sasa unapoimba mambo ambayo huna uhakika nayo haipendezi maana utakuwa hujaisaidia jamii husika alisema sugu.
 
Photo: SUGU AMSHUKIA ROMA KWA KUMTAJA KWENYE 2030:
Sugu akiwa ndani ya EATV katika kipindi cha Friday Night Live amemshukia roma na kumuonya kuwa awe mwangalifu na anachokiandika sio kukurupuka na kuandika vitu asivyokuwa na uhakika navyo.
Katika wimbo huo kuna kipande kinasema "Pesa ndio imemaliza bifu ya Ruge na Sugu"
Sugu alienda mbali zaidi na kusema madogo wanaokuja juu kimuziki hawamuwezi na ndio maana kawatafutia wa level zao ambaye ni mwanaye Sasha. Duh!
Katika nyimbo hiyo ya 2030 kuna kipande kina sema pesa ndio imemaliza vita ya ruge na sugu kitu ambacho kimeonyesha kumkera sugu na kusema kuwa roma anakurupuka na kuandika asichokijua maana kwa mstari huo tu umefanya niaamini kila achoandika hana anachokijua maana mstari huu unanihusu na hakuna ukweli juu ya alichokiimba.
 
Sugu amemtaka Roma kusikiliza nyimbo walizoimba kaka zake ili zi muongoze katika sanaa yake amesema asikize nyimbo kama za profesa jay,afande sele,solo thang atagunduwa kuwa zilikuwa ni harakati za uhakika mfano mdogo amesema asikilize miss tanzani ya solo thang atajua anachomaanisha.
 
Tulimtafuta roma kujua amejisikiaje baada ya mheshimiwa kuchukizwa na wimbo wake Roma alisema sugu ni kaka yake na anaamini kama kuna baya atamuita na atamrekebisha alipoulizwa na the superstarstz kama alikuwa na uhakika kuwa vita ya sugu na ruge imemalizwa na pesa roma alisema kimkato ndio maana hakuna tena bifu.

No comments:

Post a Comment