Friday, February 08, 2013

MWANAMUZIKI RECHO WA THT ATOWA VIDEO MPYA YA NASHUKURU


Sasa ni wakati wa kutazama video mpya ya mtoto anayetoka kwenye familia ya hali ya chini kabisa lakini Mungu amemkumbuka kwa kumshushia kipaji cha muziki ambacho sasa hivi ndio kinachangia kutunza familia yake.

Fiesta 2012 Recho aliwahi kuniambia yeye ndio anaisaidia familia yao baada ya baba yake kuanza kuugua huko nyumbani kwao Kigoma, chukua nafasi hii kufahamu huyu mrembo kaonyesha kipaji chake kwa uwezo gani kuongeza juhudi za kutengeneza pesa kuisaidia familia yake….
Hakikisha unamuunga mkono mtu wangu kwani itasaidia na yeye kuishi maisha mazuri kwa kutumia kipaji chake

No comments:

Post a Comment