Friday, February 08, 2013

                        NDOA YA AUNT EZEKIEL YAWEWESEKA.....

AUNT EZEKIELI NA  Sunday Demonte

Yule msanii mwenye taito kubwaa ndani ya bongo na nchi zilizoizunguka bongo Aunt Ezekiel  ameeonyesha kukerwa na maneno maneno ya watu aliowaita wasaga sumu wanaopakaza kuwa ndowa yake imevunjika.

Akizungumza na muandishi wetu maeneo ya mwananyamala Msanii huyo mwenye makeke kibao amesema kuwa kuna watu wanatamani leo kesho ndowa yake ivunjike ili roho zao zifurahi,aunt anasema ndowa yake imekubwa na mitihani kwani inafika kipindi watu kama wanaombea tuachane.
 
Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti, watu waliodai ni mashosti wa karibu wa staa huyo walisema wamebaini dalili za wazi kuwa ndoa yake imeyeyuka.

“Mimi ndiyo nawaambia sasa, kama mlikuwa hamjui ndoa ya Aunt haipo. Fuatilieni mtabaini ukweli wa hiki ninachowaambia.


“Nyie si mjiulize mbona tangu amerudi kutoka Dubai hajaenda tena kumfuata huyo mumewe? Si alisema amekuja kuweka mambo yake sawa kisha anakwenda kuifurahia ndoa yake, kiko wapi sasa?” alihoji mmoja wa wanyetishaji hao aliyeomba jina lake lisiandikwe gazetini.


Mwingine aliyekuwa mmoja wa waliofanikisha ndoa ya Aunt kwa kiasi kikubwa ambaye naye aliomba jina lake liwekwe kapuni alisema: 

“Hata mimi nina mashaka na hii ndoa ya huyu mwenzetu, lakini iwe imevunjika, haijavunjika sisi haituhusu, kila mtu ana maisha yake bwana.”


Katika kujua ukweli wa madai haya, mwandishi wetu alimtafuta Aunt na alipotakiwa kulizungumzia hilo alisema:


“Tuna mipango yetu mimi na familia ndiyo maana Sunday yupo Dubai na mimi huku. Sipendi kuongelea mambo ya ndoa yangu magazetini lakini kwa kifupi ipo sawa.”


 Aunt alisema yupo kwenye mipango ambayo hata mumewe anaijua na ikifika muda ataondoka kumfuata mumewe,Na kuwataka wanaomuombea mabaya wamuache kwani ndowa aliichagua mwenyewe na hakulazimishwa na mtu na kama kuacha ataacha mwenyewe na si kwa maneno ya watu.No comments:

Post a Comment