Monday, February 04, 2013

PICHA  ZA HARUSI YA  MSANII KITALE ALIPOCHUKUWA JIKO JANA

 Msanii wa Filamu za kuchekesha hapa nchini maarufu kama Kitale, jana amesherehekea siku yake muhimu, kwa kufunga ndoa na mpenzi wake, ambae leo hii tunamuongelea kama mkewe, Bi Fatma Salum.
 
Ndoa hiyo ilifungwa majira ya Saa nane mchana maeneo ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam, na kuhudhuriwa na watu kibao wakiwemo marafiki, ndugu na jamaa.KAMA tulivyoripoti siku ya Ijumaa kuwa Yussuf Mussa Kitale anaoa 
Hatimaye msanii wa vichekesho nchini tanzania Yussuf Mussa Kitale jana mchana alifunga pingu za maisha na bibie Fatuma Salum Abbas.
Kukamilika kwa tukio hilo kunahitimisha maisha ya uchumba wao wa muda mrefu tangu wakiwa shuleni na baadae kufanikiwa kupata mtoto mmoja wa kiume waliyempa jina la Hemed.
                                               

                           Bi Fatuma akiwa mtoto wao Hemed Kitale
Kwa sasa kitale ni mume halali wa bi fatuma na kwa hilo  thesuperstarstz inampongeza sana kitale na mkewe bi fatuma kwa kuamua kufanya jambo hili jema na la kumpendeza mungu, nawaombea  ili muweze kumlea hemedy katika njia impendezayo mungu.

No comments:

Post a Comment