Monday, February 04, 2013


PICHA ZA MOTO MKUBWA ULIPOTEKETEZA VIBANDA KWENYE STENDI YA MWENGE DARLeo kumetokea moto ulioteketeza vibanda kadhaa vya biashara katika stendi ya Mwenge jijini Dar es Salaam.

Akiongea na waandishi wa habari, Kamanda wa polisi mkoa wa kipolisi wa Kinondoni Charles Kenyela amesema moto huo umeteketeza frame kadhaa husasan mbili lakini umedhibitiwa na kikosi cha zimamoto, wananchi na jeshi na polisi.

“Mali nyingi zimeokelewa lakini kwasababu ya hali halisi zingine zimeharibika sababu ya muda na ile kadhia ya kukanyagana wale waliokuwa wanaokoa hawajafanikiwa kuokoa vyote, “ alisema.

“Hakuna madhara kwa binadamu na tunashukuru kwamba moto umetokea mchana lakini vinginevyo kama ingekuwa ni wakati wa usiku hali ingekuwa mbaya sana.”

Chanzo cha moto huo kinadaiwa kuwa ni hitilafu ya umeme.
Bidhaa zikiwa zimeokolewa

Bidhaa zikiwa zimeokolewa
IMG_3876 (640x427)
IMG_3875 (640x427)
IMG_3868 (640x427)
IMG_3869 (640x427)

Baadhi ya vitu vilivyoungua
Baadhi ya vitu vilivyoungua

IMG_3850 (640x427) - Copy

IMG_3847 (640x427) - Copy

IMG_3843 (640x427)
IMG_3840 (640x427) - Copy
IMG_3838 (640x427)
Gari la zimamoto
Gari la zimamoto

No comments:

Post a Comment