Tuesday, February 05, 2013

PREZZO NA GOLDIE KUFUNGA PINGU ZA MAISHA FEBRUARI 9Kwa mujibu wa mitandao mbalimbali nchini Nigeria, rapper Jackson Makini aka Prezzo anatarajia kufunga ndoa na mwanamuziki wa Nigeria Goldie February 9.


Habari hiyo pia imeandikwa na website ya Big Brother Africa. Harusi hiyo itafanyika jijini Lagos, Nigeria.

Katika hatua nyingine mwakilishi wa mwaka jana wa Nigeria kwenye shindano la Big Brother Africa, anatarajia kuanzisha Reality TV show yake.Goldie anaanzisha show hiyo iitwayo ‘Tru Friendship’. ‘Tru Friendship’ itaonesha maisha ya kila siku ya muimbaji huyo wa Skibobo, Goldie, yote kama mtu maarufu na kama Susan Harvey.

Show hiyo itaanza kuonekana mwishoni mwa mwezi huu.

No comments:

Post a Comment