Friday, February 15, 2013

RAIS KIKWETE ASAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO, ATOA HESHIMA ZA MWISHO KWA MAREHEMU ASKOFU THOMAS LAIZER
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akitia saini kitabu cha maombolezo ya Askofu Thomas Laizer wa Dayosisi ya Kaskazini Kati la Kanisa la Kiinjili cha Kilutheri Tanzania (KKKT) leo, Alhamisi, kwenye Kanisa Kuu la KKKT mjini Arusha kabla ya kutoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa Askofu. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akitoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa Askofu Thomas Laizer wa Dayosisi ya Kaskazini Kati la Kanisa la Kiinjili cha Kilutheri Tanzania (KKKT) leo, Alhamisi, kwenye Kanisa Kuu la KKKT mjini Arusha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiifariji familia ya Askofu Thomas Laizer wa Dayosisi ya Kaskazini Kati nyumbani kwa Askofu mara baada ya kuwa ametoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa marehemu kwenye Kanisa Kuu la KKKT mjini Arusha leo, Alhamisi, Februari 14, 2013. Picha zote na Fredy Maro wa Ikulu

No comments:

Post a Comment