Tuesday, February 19, 2013

"SINA KINYONGO JUU YA PENZI LA DIAMOND NA PENNY"...JOKATE

BAADA ya Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kupata demu mpya, Penniel Mungilwa ‘Penny’, Jokate Mwegelo ametoa baraka zake kwa jamaa huyo aliyewahi kudaiwa kuwa mpenzi wake akisema haoni tatizo wawili hao kuwa pamoja kama kweli wamependana na kuridhiana.
 
 
Akizungumza katika mahojiano maalum alipobanwa kuhusiana na uhusiano wa wapenzi hao huku ikifahamika kuwa Penny alikuwa shosti wake, Jokate ambaye ni Miss Tanzania namba 2, 2006/07 alisema kwamba yeye na mrembo huyo walikuwa washikaji tu na wala hawakuwa na urafiki wa karibu kama baadhi ya watu wanavyoamini.
 

Jokate ambaye pia ni mtangazaji wa Runinga ya Channel O alifunguka kuwa anawatakia kila la heri na baraka zote Diamond na Penny katika uhusiano wao mpya wa kimapenzi endapo tu watakuwa wamependana na kuridhiana kwa dhati.

“Japokuwa sipendi kumuongelea Diamond lakini ukweli sioni tatizo kwa wao kupendana, mimi naona poa tu,” alifunguka Jokate ambaye pia ni bonge la mwigizaji.

Kabla ya kutoka kimapenzi na Penny ambaye naye ni mtangazaji wa Runinga ya DTV, Diamond aliwahi kuviteka vyombo vya habari akiripotiwa kuwa na Jokate, kabla ya mambo kwenda mrama.

No comments:

Post a Comment