Saturday, February 09, 2013

"SINA NDOTO YAKUOA MSANII YEYOTE....TULIZO LA MOYO WANGU NI MFANYAKAZI WA BENKI"....RAY WA BONGO MOVIE

KATIKA kile kilichotafsiriwa kuwa ni kuwafutilia mbali wasanii wenzake, Blandina Chagula na Ruth Suka ‘Mainda’ aliowahi kudaiwa kutoka nao kimapenzi, staa wa filamu Bongo, Vincent Kigosi amefunguka kuwa, hatarajii kuoa msanii kwani anaogopa presha.

Akizungumza issue hii hivi karibuni, Ray alisema kuwa anajua matatizo ya kuoa staa hivyo ili kuepukana nayo ameamua kuwekeza penzi lake kwa mwanamke anayefanya kazi benki akidai kuwa huyo ndiye tulizo la moyo wake.“Kaa ukijua kuwa sina mpango wa kumuoa staa yeyote, mwanamke ninayetarajia kumuoa ni mfanyakazi wa benki na mipango yangu ikikamilika nitakueleza kila kitu. Mimi sitaki presha bwana,” alisema Ray.The superstars ilimtafuta johari maeneo ya mbezi alipokuwa anashuti filamu yake mpya na kumhoji juu ya swala hilo na kusema yeye hana mahusiano na ray kwa hiyo haoni sababu ya kuhojiwa kwa hilo mimi ray ni mkurugenzi mwenzangu sasa ninashaka kuja kunihoji mimi sina mahusiano nae alisema johari.
Hatukuishia hapo tulimtafuta mainda ambaye alijibu kwa kifupi kuwa yeye kwa sasa ameokoka na anampenda yesu kwani ndiye msimamizi wa maisha yake kwa hiyo asingependa kutafutwa kwa ajili ya mambo kama hayo  kwani muda wake mwingi anautumia kwenda kanisani na kusoma bibilia No comments:

Post a Comment