Tuesday, February 12, 2013

VURUGU ZILIZOTOKEA GEITA KATI YA WAISLAM NA WAKRISTO. ZIMESABABISHA HASARA KUBWA NA KUACHA MAJERUHI KIBAOMajeruhi Abdalah Ibarihim akiwa amejeruhiwa vibaya baada ya kukatwa mapanga kichwani na watu wanaodaiwa kuwa ni Wakristo.Huyu naye ni majeruhi aliyetambuliwa kwa jina la Steven Andrea (34) ambaye anadaia kujeruhiwa na watu wanaosadikiwa kuwa ni waislamu.Wadau nianze kwa kusema nasikitika sana kwa haya yanayotokea kwani hakuna kitu kibaya kama vita na hasa vita ya imani,nashindwa kuelewa serekali yetu makini ipo wapi hadi tunafikia hatua hii ya kupigana mapanga kisa kikiwa ni dini.Nalazimika kuandika kwa uchungu kwani na amini tunajivuna kwa kuwa hatujawahi kuingiwa na mdudu  vita lakini kama tukitaka kujua ubaya wa vita tuwaulize ndugu
zetu,Somalia,Rwanda,Burundi,Kenya,watatuambia nini maana halisi ya neno vita,ninachowaomba ndugu zangu tujitaidi kuitunza na kuilea hii amani kidogo tuliyo nayo kwani ikitoweka yatakuwa majuto kwa wengi furaha kwa wachache,, thesuperstarstz inawapa pole sana wale wote waliojeruhiwa ama kuharibiwa mali zao na inawataka wawe na moyo wa subira kama mwenyezi mungu anavyotuelekeza katika vitabu vyake kuwa kila mwenye subira yupo pamoja nae.

No comments:

Post a Comment