Thursday, February 14, 2013

       MSANII WA KUNDI LA TMK WANAUME HALISI AFARIKI DUNIAMsanii wa kundi la Wanaume Halisi linaloongozwa na Juma Nature , Baraka Masale Sekela aka BK, amefariki dunia Jana asubuhi.


Kwa mujibu wa blog ya Sam Misago wa East Africa Radio, taarifa hizo zimetolewa na member wa kundi hilo la TMK Wanaume Halisi, Rich One.

Amesema sababu za kifo cha BK ni matatizo ya tumbo na ini yaliyokuwa yakimsumbua kwa muda mrefu.

Thesuperstarstz inaungana na ndugu jamaa na marafiki na watanzania wote katika kipindi hichi kigumu cha kumpoteza ndugu yetu,Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi...Amen

No comments:

Post a Comment