Wednesday, February 20, 2013

WASICHANA WATANO WANAOJUA KUTUNZA STEJINI

 Tasinia ya filamu nchini inakuwa kwa kasi na kuwafanya wasanii wa anze kumiliki mkwanja na kujikuta na wao kwa njia moja au nyingine wanazitunza familia zao na kuwasaidia pia wasiokuwa nacho katika matatizo

Orodha hiyo hapo hini ni orodha inayohusu wale wasnii wenye moyo wa kujitolea kwa wenzao na ambao kwa sasa wanamiliki mkwanja mrefu na mara nyingi wamekuwa wakiwa tunza sana watu linapokuja swala la sherehe yoyote.


NO (1)
Wema Sepetu
Msanii huyu ametajwa kuwa ni msanii wa kwanza kwa sasa anayemiliki mkwanja mrefu kutoka bongo movie huku akimiliki magari ya kifahari kama Q 7 AUDI na Mark X pia ana miliki ofisi ya kisasa ambayo hakuna kama hiyo katika wasanii ni ofisi ya kwanza kwa uzuri katika wasanii.

Thesuperstarstz imekuwa akimfuatilia kwa kina mwanadada huyu na kubaini kuwa pamoja na utajiri wote huo pia ni msanii anayependa kutowa sana misaada kwa maskini na kwa wale ambao kwa namna mmoja  nyingine wamepoteza matumaini.pia imefahamika kuwa wema ni kati ya wasichana wanaopenda sana kutunza watu katika kumbi mbali mbali za disko,maharusini,bithday,na kichen pati hii inatufanya kumpa namba moja kwakuwa hata wasanii wenzake wamekiri kuwa wema anawazidi kwa pesa na ni wa kwanza pia kwa kutunza,huku wengine wakisema dau la wema  kulifikia ufanye kazi.alisema msanii mmoja jina kapuni

         NO (2)
Yobinesh Yussuph (Batuli)
Mwanadada huyu kwa sasa anafanya poa sana katika filamu za bongo na ni kati ya wanawake wanaomiliki mikwanja mirefu sana huyu alianza kungaa sana pale alipoigiza fake smaile na marehemu kanumba na kusababisha sauti yake na ya kanumba kutumika kama milio ya simu pale walipokuwa wanaongea na simu.

Kwa taarifa za mtu wetu wa karibu mwanadada huyu  amekuwa akionekana na mgari ya kifahari na inasemekana ana mikakati mizito ya kukamilisha nyumba alioiita ikulu yake na kwasasa ana kamilisha ujenzi wa ofisi yake ya kifahari japo chanzo chetu hakikusema ofisi hiyo itakuwa inajishughulisha na nini.

Kwasasa msanii huyu amechaguliwa kuwa balozi wa amani nchini tanzania kupitia taasisi inayojihusisha na maswala hayo katika kipengele cha mama na mtoto youth cross cultural & Environmental conservation.

Batuli amekuwa akikaririwa na vyombo kadhaa vya habari akisema ana umizwa sana anapoona vifo vya mama na mtoto vikiendelea kutokea ,msanii huyu ni mmoja kati ya wasanii ambao wanajua kujitowa kwa wenzao na wanaojua kutunza iwe katika harusi,kichen pati,mahafali,bithday pati na Nk.

 Habari hii ni kwa mujibu wawasanii wenzake ambao wanamsifu sana kwa moyo wa kujitolea na kuwa na huruma kwa binadamu wenzake pia wamemtaja kama mwanamke anayebadili magari ya kifahari kila kukicha mara vogue spot,shangingi, na mengine mengi.


NO (3)

Jackline Wolper

Kwa sasa mwanadada huyu ni kama katulia vile kwani zile kashi kashi zake hazionekani tena kuna kipindi alitajwa kumiliki mkwanja mrefu sana ila kwasasa ni kama anajipanga upya ila bado anashika nafasi ya juu kama si ya kwanza katika soko la filamu nchini tanzania

Ni ukweli usiopingika kama jack kwa sasa hakamatiki sokoni kwani amekuwa lulu kwa jinsi anavyosakwa na wa nunuzi wa filamu husika na kusababisha watengenezaji wahangaike kumpata mwanadada huyo.

Kwa upande wa mkwanja bado jack yupo vizuri kwani ana miliki vitu kibao yakiwemo magari na viwanja kibao,mwanadada huyu pia ametajwa kuwa miongoni mwa wasichana wa bongo movie wanaopenda sana kujitowa na kutunza kama mtakumbuka alitowa milioni kumi na tano katika kusaidia matibabu ya marehemu sajuki ukiachilia mbali pesa anazomwaga wakati wa sherehe mbali mbali .


NO (4)

Halima Yahaya (Davina)
Huyu ni msanii anayefanya vizuri sana kwa sasa na ni kati ya wasanii wenye roho nzuri sana na mwepesi kujitowa kwa hali na mali,Davina anajitowa sana katika shida utamuona na katika raha pia utamuona

Mwanadada huyu ametajwa pia katika orodha ya wanawake wa bongo movie wanaotowa sana mkwanjwa kwa kuwa tunza watu katika sherehe za kichen pati au harusi.


NO (5)

Irene Uwoya
Ni mwanamke ambaye huwa hapendi kukaa na gari moja ni mtu wa kumiliki na kuuza ni mtu ambae anapenda sana kila gari jipya aliendeshe,mwanadada huyu kama ilivyo kwa wengine ameshacheza filamu nyingi sana ambazo zimemuingizia kipato kikubwa sana na kumfanya amiliki mkwanja wa kutosha

Kama kawaida yake amekuwa mtu anayeamini kuwa maisha ni zaidi ya kile unachokiamini kwani huwa hawezi kukaa kipindi kirefu bila kwenda kwa watoto yatima na  kwa omba omba hii yote ni kuonyesha utu na hivi karibuni the superstars page ili ripoti habari ya mwanadada huyu kuamua kusheherekea sikuku yake ya kuzaliwa kwa kuwatembelea wagonjwa wa mwanananyamala hosptali na kutowa misaada kwa wagonjwa,


Tafadhali tunarejea tena kusema kila kilichoandikwa hapa ni kwa mujibu wawasanii wenzao walipohojiwa na kuwaelezea  wasanii hao kuwa ni wepesi wa kutowa na kuisaidia jamii na ni ma bingwa wa kutunza.

No comments:

Post a Comment